USHAURI UNAPOENDA KUNUNUA SIMU MPYA

Related image

Kama tujuavyo miaka ya hivi sasa kumekuwa na mapinduzi ya ajabu ya ki teknolojia haswa kwenye upande wa simu zetu za mkononi. Sasa unapoenda kununua simu ili uende na teknolojia ya kisasa ni lazima ufahamu simu unayoenda kununua inatakiwa iwe na sifa gan au na vitu gani. Zingatia yafuatayo
#Teknolojia_mpya
Tunapozungumzia teknolojia mpya hapa tunaanzia nje ya simu hadi ndani ya simu. Sasa ili uweze kuwa na simu ya kisasa lazima uhakikishe unanunua cm yenye teknolojia ya kisasa.
Kwa ushauri hapa usinunue simu yenye android 5.0 kushuka chini, yaani tafuta simu yenye android 6.0 na kuendelea.
Kwanini?
Hii ni kwasababu matoleo ya android yanazidi kutolewa kila mwaka na yale ya zamani yanaondolewa hivyo watengenezaji wengi wa programs(apps) wanatowa apps zao kutokana na teknolojia jinsi inavyokwenda na ndo maana unakuta kama simu yako ina android version ya kizamani basi utakuta kuna baadhi ya app za kisasa hazifanyi kazi katika simu hiyo.
#Uwezo_wa_RAM
Hiki ni kitu muhimu sana pia. Watu wengi wanapokwenda kununua simu huwa hawaangalii uwezo wa RAM wa simu hyo badala yake ataangalia camera basi😂(selfie addicted). Ili kuepuka kwa simu yako ku stack mara kwa mara… Mara unashangaa inajifungua ma apps bila ya wewe kufungua mara nyingi matatizo kama haya hujitokeza baada ya RAM kuzidiwa.
Hivyo basi tunarudi kwenye hyo point ya mwanzo kabisa unaponunua simu ya kisasa basi lazima itakuwa na uwezo mkubwa wa RAM tofauti na matoleo ya Kizamani. Kutokana na teknolojia basi hata apps zinazotengenezwa kutokana na usasa wake basi zinakuwa zinahitaji nafasi kubwa kiasi katika RAM ili ziweze ku RUN ipasavyo hvyo kama utanunua simu yenye uwezo mdogo wa RAM basi utaambulia ku stack stack kwa simu. Kumbuka uwezo wa RAM hulandana sana na uwezo wa Processor kama nlivyokwishaga kutowa post inayohusiana na processor. Kwahvyo RAM ikiwa kubwa lazma na processor yako itakuwa na uwezo mkubwa pia kama RAM yako ndogo basi lazma na ka proccessor chako katakuwa kadogo.
#Ukubwa_na_uwezo_wa_kioo
Ukubwa na uwezo wa kioo hapa unaweza kuona labda sio kitu cha muhimu lkn ngoja nkwambie kwanini ni muhimu.
Kwa upande wa kioo mara nyingi uwezo wa kioo chako unategemea sana kudumu kwa simu yako. Unakuta umenunua simu ndani ya wiki moja tu umeangusha na kimevunjika hii ni kutokana na teknolojia ya kioo chako. ( najuwa bado unatowa macho hujaelewa😂😂😂)
Hapo namaanisha hvi mara nyingi vioo vya simu za zamani huwa ni vyepesi sana kupasuka kwasababu kipindi hicho makampuni ya utengenezaji simu yalikuwa bado hayajapa ufumbuzi au yalikuwa hayajagundua juu ya utengenezaji mpya wa vioo bora zaidi ili kutatua tatizo la simu kuvunjika udoshapo kidogo tu hvyo kama tunavyojuwa teknolojia inavyozidi kwenda ndvyo na wao wanavyozidi kuboresha zaidi mambo yao.
Kwa upande wa ukubwa wa vioo hapa mara nyingi watengenezaji wa programs za android hutengeneza program zao kwa kulenge vioo vikubwa kutokana na teknolojia ilivyo sasa( hapa watu wanaoelewa Mambo ya graphics basi wananielewa zaidi). Hii ni kwasababu kwa sasa hakuna simu yoyote inayoingia sokoni ikiwa na kioo kidogo hivyo pale unapoenda kununua simu ni vema ukachagua simu yenye kioo kikubwa kwa wastani ili kuendana na teknolojia jinsi inavyokwenda.
#Uwezo_wa_battery
Hapa sikatai wengi wamekuwa wakizingatia sana kuangalia uwezo wa battery lakini wamekuwa wakiangalia kwa utofauti. Yaani mtu anaulizia battery linakaa na chaj masaa mangapi badala ya kuangalia uwezo kamili wa battery. Jua kwamba simu kukaa na chaji masaa kadhaa na uwezo wa battery ni vitu viwili tofauti kabisa( nataka kutoa mfano ila nimechoka kuandika jifkilie menyewe utaelewa mbele kwa mbele na ukielewa weka comment wenye kutoa macho waelewe pia😂😂).
Hvyo basi wakati unanunua simu unatakiwa uangalie uwezo halisi wa battery lako na sio kuuliza inakaa nachaj muda gani. Hapa unatakiwa kuangalia #milliampere_hour(mAh) hiko ndo kipimo unachotakiwa kuangalia ili kujua uwezo wa battery yako.
Hii mAh unaingalia kwenye boxi la simu yako au kama simu haitakuwa na boxi basi iangalie kwenye battery lenyewe utakuta imeandikwa (mfano 3800mAh).
Hivyo basi unapoenda kununua simu usiulize inakaa na chaj muda gani badale yake soma hiko kipimo na kwa teknolojia ya sasa battery ambayo ni nzuri inaanzia 2500mAh na kuendelea kwa battery zenye uwezo kuanzia hapo zitakusaidia kutimiza mambo yako mengi na kudumu na chaji kutokana ma matumizi yako.
#Mengineyo
Hapa kwenye mambo mengine ya kuangalia wakati unanunua Simu yako ambayo sio msingi kiviiile mana hapa inategemea na mnunuaji sasa unatakaje ni kam Vile mambo ya ulinzi wa simu yako may be unataka iwe na finger print, mara cjui camera ianzie mega pixel 13 nakuendelea aaah hayo sio muhimu saaana mana kitu tunaangalia kwa sasa ni simu inapigaje kazi… Mziho unatakiwa uwe na speed ya ajabu ukibofya tu imooo😂😂😂… Anyway ebu tuishie hap


Usisahau kushare post hii.👍 Share facebook, twitter, Google+ n.k bila kusahau WhatsApp! Share kote wenzio nao wasome

 

  🔞Wakubwa tu: video kali zote na original app download chini
TAHADHARI WAKUBWA PEKEE NDIO WANARUHUSIWA KUBONYEZA HII LINK WATOTO KAA PEMBENI



No comments:

Powered by Blogger.