Faida na umuhimu wa kutofanya Tohara
Faida wanazopata wanaume ambao hawajafanyiwa tohara
1.Uume wenye urefu na upana kamili
Govi linachangia asilimia 50 au zaidi katika mfumo wa ngozi ya uume.Kama likikunjuliwa na kutandandazwa kwa kunyooshwa. litafikia sentimita za mraba 60 mpaka 90(inchi za mraba 10 mpaka 14).Govi linaufanya uume kuwa mrefu hasa ikiwa govi ni refu kupita kichwa cha uume. Wakati uume unapokuwa unasimama govi hujaa damu na kufanya uume na kichwa cha uume kuongezeka unene.Wakati govi lililojaa damu linapojivuta na kuvuka coronal ridge(sehemu iliyoinuka na yenye upeleupele inayozunguka kichwa cha uume) ya kichwa cha uume kunakuwa kunatengenezwa na kufanya sehemu ya kusisimulia/kusisimuliwa (colonal ridge) kuwa pana zaidi ambapo wapenzi huwafanya wapate stimu wakati wa kusex. Uume uliotahiriwa huonekana umepunguzwa na mwembamba kuliko uume usiotahiriwa ulio na urefu kamili .
2.Ulinzi.
Govi linafunika kichwa cha uume na kuzuia mikwaruzo,kukauka,kukakamaa ,kuzuia vitu vinavyoweza kusababisha maambukizi kutoka mazingira ulipo. Kichwa cha uume kinategemewa/kinapaswa kulindwa kwa viuongo vya ndani vya mwanaume kama ilivyo kwa kisimi kwa wanawake. Athari kwa kichwa cha uume ulio wazi katika kukakamaa kwenye mapenzi hazijawahi kufanyiwa utafiti. Taarifa nyingi kwa wanaume waliotahiliwa zinaonyesha kuwa msisimko wa kufanya mapenzi, raha unapungua.
3.Ridged bands(govi kwa ndani lina sehemu ijulikanayo kama ridged bands).
hii ni sehemu muhimu inayosababisha raha inapoguswa ama kugusika kwa wanaume na kusababisha mwitiko wa kimapenzi/mapenzi.
kwa kiswahili.
4.Gliding action(kitendo cha kuteleza)
Govi ni sehemu pekee inayoweza kuteleza kwenye uume. wakati wa kufanya mapenzi govi na kichwa cha uume vinafanya kazi pamoja na mujumuiko huu unatengeneza mwitiko kamili wa mapenzi. kitendo cha mtelezo kati ya govi na kichwa cha uume katika kufanya mapenzi wakati wa kuingiza na kutoa uume ndani ya uke kinaweka mazingira kwa tendo kuwa zuri na la raha kwa wapenzi.Bila mtelezo huu, uume uliofanyiwa tohara unafanya kazi ya kutoa nje vilainishi vilivyomo ndani ya uke wa mwanamke na kuvitoa nje kwenye upepo/hewa kavu na hivyo kufanya matumizi ya vilanishi vya kufanyia mapenzi kuwa na matumizi rasimi ili kuzuia maumivu wakati wa tendo kwa wanaume waliotahiriwa.
5.uwepo wa mishipa ya hisia
kwa kuongezea kama ilivyoelezwa awali kwenye ridged band, maelfu ya meissner's corpuscles(mishipa ya hisia za mapenzi) yanabeba sehemu muhimu zaidi ya mishipa ya hisia za uume. Govi lina mishipa ya hisia kati ya aina 10,000 na 20,000 ambayo ni maalumu kwa hisia za mapenzi ambayo ina uwezo wa kusababisha kuhisi hata kwa mguso mdogo tu , kuhisi mabadiliko kidogo ya joto na hata kuhisi mguso kidogo tu wa ngozi nyororo.
6.Frenulum(mshipa)
Hii ni sehemu yenye uwepo mwingi zaidi wa mishipa ya hisia inayounganisha govi na sehemu ya chini ya kichwa cha uume.Hii sehemu ni sawa na mshipa wa chini ya ulimi, pia ni sawa na mshipa uliopo ndani kwenye lips ya juu katika mdomo na pia ni sawa na mashavu ya uke wa mwanamke.. Kwa wanaume wengi wenye govi sehemu hii ni sawa kabisa na G-spot iliyopo kwa wanawake na sehemu hii inasisimka zaidi inapovutika na kusinyaa kwa kadiri unapoingiza na kutoa uume kwenye uke(pumping).Wakati wa tohara sehemu hii huharibiwa kiasi ama huharibiwa kabisa kutegemea na njia itakayotumika kufanya tohara.
Kwa Kiswahili.
7.Mzunguko stahiki wa damu kwenye uume.
Govi lina mishipa baadhi ya damu ikiwemo FRENULAR ARTERY na matawi ya DORSAL ARTERY. Upotevu wa mishipa hii kwa njia ya tohara inasababisha mfumo wa damu kuzunguka kwenye uume na kichwa cha uume kuharibiwa na kuharibu kabisa MATUMIZI HALISIYA UUME pamoja na kuathiri ukuaji ama kujengeka kwa uume.
8.Mfumo wa kujilinda na maambukizi mbalimbali.
Majimaji ndani ya govi yanatoa seli zinazozalisha mfumo wa ulinzi kwa kuzalisha seli za ulinzi,pia seli za kupambana na bacteria na seli za kupambana na virusi. Mathalani enzemu zinazoua viambukizi vya magonjwa. Na kwa ujumla majimaji yote katika mwili wa binadamu ikiwemo yanayopatikana kwenye kuta za macho,uke,mkundun na kwenye govi ni sehemu muhimu na za kwanza kwa mfumo wa ulinzi wa mwanadamu dhidi ya shambulio lolote la maambukizi na magonjwa. Faida ya govi inaweza kuelezwa kama moja ya sababu muhimu ya kwa nini wanaume wenye magovi wapo katika hatari ndogo zaidi ya kuambukizwa ugonjwa wa Chlamydia na magonjwa mengine ya zinaa.
9.Langerhans cells.
Hizi ni seli zinazotengeneza sehemu ya mfumo wa ulinzi wa mwanadamu na zinaweza kutumika kuzuia/kukinga uume usiambukizwe na magonjwa ya zinaa kama UKIMWI.
10.mzunguko stahiki wa limfu.
Govi lina mishipa ya limfu ambayo ni muhimu kwa usambaaji wa limfu na kazi ya kiulinzi.
11.Estrogen receptors.
Govi lina estrogen receptors ambazo mpaka sasa hazijafanyiwa utafiti wa kina na kunahitajika utafiti wa kina kujua kazi zake.
12.Apocrine glands.
Vifuko hivi huzalisha pheromones, viashiria asilia kwa wapenzi, Athari za kutokuwepo kwa vifuko hivi katika tabia za mapenzi hazijawahi kufanyiwa utafiti.
13. vifuko vya Sebasiasi.
Huzalisha mafuta ya kulainishia govi na kichwa cha uume ili kwa pamoja vitu hivi vifanye kazi kwa pamoja vizuri.
14.Mshipa wa chini ya uume.
Huu ni mshipa unatokea kwenye korodani mpaka kwenye govi chini ya uume. Kazi yake ni kudhibiti kiwango cha joto linalotakiwa kwenye uume na korodani kwa ajili ya uzalishaji wa mbegu ambapo wakati wa joto , uume huongezeka urefu ili kuruhusu joto kupungua na wakati wa baridi, uume husinyaa ili kuzuia joto zaidi kupote . Baada ya tohara inakadiliwa karibu nusu ya mshipa huu huharibiwa(NB kwa aina ya tohara ya wamasai sehemu hii haihariki maana huwa hawakati sehemu ya chini, wao huita fagio)
15. Muonekanohalisi na rangi ya kichwa cha uume.
Kwa wanaume ambao hawajafanyiwa tohara, kichwa cha uume huwa nyevunyevu,king'aacho na rangi yenye mchanganyiko wa pink na nyekundu kelekea kwenye weusi na dhambalau.
Muonekano huu unamvutia mpenzi. Kichwa cha uume ulifanyiwa tohara kinaonekana rough na kilichokauka kikiwa na rangi ya pink nyepesi kuelekea rangi ya mchanganyiko wa bluu na kijivu.
16. Kukwepa hatari yoyote ya maambukizi hatari ama athari na ajari ya tohara.
Kwa bahati mbya vijana ambao hujikuta katika tohara zilizokosewa ama kufanywa vibaya hujikuta wakipoteza sehemu ya uume wao ama uume wote kwa sababu ya makosa yanayoweza kufanywa katika kutahiri ama kwa maambukizi . mara nyingi wanafanyiwa mabadiliko ya jinsia kwa kuhasiwa ama kubadilishwa jinsia.na wanalazimika kuishi kama wanawake kwa kuwa kudungwa dozi ya homoni lakini hata hivyo hili halijaweza kufakiwa kwa kiwango stahiki
17. Kukwepa hatari yoyote ya kifo kitokanacho na tohara.
Kila mwaka vijana wanafariki kutokana na makosa yanayofanywa kwenye tohara , ukweli ambao Mamlaka za tohara nchini Marekani zinaupuuza,kuuzima/kuuzuia ama kuupa nafasi ndogo.
No comments: