Enyi wanaume msiwe na tabia kama za mume wangu

Image result for namani mwanaume mwenye uwezo wa kunisugua

Nimeolewa na nina mtoto 1 wa 5yrs, mwanzo wa ndoa yetu tulikuwa na maisha ya chini ndugu wa mume waliniheshimu nami niliwaheshimu, MUNGU akatujalia rizki tukajenga na tukafungua biashara, mawifi (Wamachame)wote wameolewa na wanamaisha mazuri wakaanza tabia ya kuja kwangu ghafla kwa wakati tofauti bila taarifa na wananiambia naomba laki 5,6 nitarudisha, inabidi nijipigepige niwape nikatoa km mara 3 .

Mwisho akaja mmoja kutaka nimpe kaki 8 atarudisha nikamuuliza mbona hajarejesha ile hela nyingine aliyonikopa? hapo ndo wakaanza kunipiga vita na kumwambia mdogo wao "mume wangu" kuwa mimi simfai eti kwanini nawanyima hela. 

Wakati ni za ndugu yao, na mume wangu akaanza kunichukia, nikimwelewesha haelewi amenimbia hataishi na mimi kama mke wake na hatajishughulisha na mtoto aliye tumboni mwangu kwa sababu sitaki kuwafanyia dada zako chochote wanachotaka.

HUU NI MWEZI WA 2 UNAISHA HAJAWAH KUNIULIZA CHCHT JUU YA MAENDELEO YANGU WL MWANAE TUMBONI ila mara 3 sasa anaamka usiku analia na kumuomba MUNGU AMSAMEHE, NIFANYAJE MIMI?

No comments:

Powered by Blogger.