NAMNA YA KUOGA HEDHI NA NIFASI.....
Kuoga hedhi na nifasi ni sawa sawa na kuoga janaba lakini kuna baadhi ya mambo yanaongezeka na kutofautiana:
nia ama ya hedhi au nifasi.
2.Ataosha mikono yake, halafu atajisafisha sehemu zake siri vizuri.
3.Atajitia udhu wa Salaa bila kumalizia miguu.
4.Ataosha kichwa chake kwa kutumia ama sabuni au shampoo, maji atayasugua mpaka yafike kwenye mizizi ya nywele.
5.Ataosha mwili mzima na kujisugua kwa kuanzia kulia halafu kushoto.
Hadithi ya Bibi Aisha R.A. kasema,
"Bibi Asma bint Yaziid alimuuliza Mtume S.A.W.
"Bibi Asma bint Yaziid alimuuliza Mtume S.A.W.
namna ya kuoga hedhi akamjibu kwa kusema
"Atachukuwa mmoja wenu maji na sidra (sasa sabuni na shampoo) halafu atajitia udhu wa Swalaa atajisafisha kichwa chake, atajisugua vizuri mpaka maji yafike kwenye mizizi ya nywele zake, halafu atajimwagia maji mwili mzima.
Halafu atachukuwa pamba na atajisafisha nayo.
" Akamuuliza Bibi Asma,
"Vipi kujisafisha kwa hiyo pamba."
Akasema Bibi Aisha R.A...
Akasema Bibi Aisha R.A...
“Nilifahamu nini alikusudia Mtume S.A.W.
nikamwambia
"Utasafisha mabaki ya damu kuondoa harufu yake."
No comments: