KUKOSA MSISIMKO WA TENDO LA NDOA KWA WANAWAKE
Kukosa msisimko wa tendo la ndoa kwa wanawake-
(Female Sexual Arousal Disorder -Fsad)
WANAWAKE wengi wanasumbuliwa na tatizo la kukosa msisimko lakini kwa bahati mbaya, ni wachache wanaofahamu tatizo linalowasumbua ni nini. Kwa kifupi, hii ni hali ambayo mwanamke anakosa kabisa msisimko na raha ya tendo la ndoa.
Dalili za awali za tatizo hili, ni kama ifuatavyo:
-Kulifikiria tendo la ndoa mara chache zaidi (mwanamke hafikirii mara kwa mara kuhusu tendo la ndoa).
-Kutosikia raha yoyote, kabla, wakati wa tendo au baada ya tendo. Yawezekana mwanamke akawa hasikii maumivu yoyote lakini pia anakuwa hahisi tofauti yoyote.
-Mwanamke kuanza kukataa kushiriki tendo, yawezekana awali alikuwa akikutana na mwenzi wake mara kwa mara lakini ghafla ratiba zinabadilika na hahisi tofauti yoyote.
-Kupoteza kabisa msisimko wa mapenzi. Inapofikia hatua hii, hata kama mwanamke atawekwa kwenye hali ambayo ni rahisi kupata hisia, hushindwa kufanya hivyo.
Zipo sababu nyingi zinazosababisha tatizo hili, na sababu hizo zinawekwa katika makundi mawili, za kimaumbile na za kisaikolojia.
Tafiti za kitaalamu, zinaonesha kwamba matatizo ya kisaikolojia huanza hasa baada ya mwanamke kuvunja ungo ambapo mwili huanza kuzalisha homoni ambazo huubadilisha mwili kimuonekano na kihisia.
Homoni hizi zinapozalishwa kwa kiwango kinachostahili, humfanya mwanamke awe na hisia za kawaida kama watu wengine lakini kunapotokea athari yoyote katika uzalishwaji wa homoni hizi, hapo ndipo tatizo huanzia.
Wanawake waliopitia unyanyasaji wa kijinsia wakiwa wadogo, pengine kwa kubakwa, kuteswa kingono, kuteswa kihisia au kunyanyaswa, nao wapo kwenye hatari kubwa ya kupatwa na tatizo hili ukubwani.
Matatizo ya msongo wa mawazo, kusalitiwa kwenye uhusiano wa kimapenzi, kunyanyaswa na mume na uchovu wa kupitiliza (fatigue), husababisha tatizo hili. Kutazama picha za ngono kwa kiwango cha kupitiliza ni tatizo lingine.
No comments: