TATIZO LA KUTOPATA RAHA WAKATI WA TENDO LA NDOA
TATIZO LA KUTOPATA RAHA WAKATI WA TENDO LA NDOA
_Wapo ambao wakati wanapofanya mapenzi badala ya kupata raha, husikia maumivu, mwanaume katika uume lakini ni mara chache sana kulinganisha na wanawake._
_Mwanamke ndiye husumbuliwa zaidi na tatizo hili._
_Mwanamke anaweza kukosa raha kabisa na matokeo yake kuumia wakati tendo linapoanza pale mwanzoni ukeni au kwa ndani zaidi._
_Maumivu haya pia yanaweza kugawanyika katika makundi mawili._
Kwanza maumivu wakati wa tendo mbayo ndiyo hayo tuliyoyaona hapo juu na maumivu baada ya tendo._
*Kuumia wakati wa tendo*
_Maumivu haya hutokea pale uume unapoanza kuingia ukeni na hutokana na uke kuwa mkavu._
Hili linaweza kusababishwa na maandalizi duni kabla ya tendo, matatizo katika mfumo wa homoni au kupoteza msisimko na hamu ya tendo._
_Kubana kwa misuli ya uke pia huchangia ingawa tatizo hili zaidi ni la kisaikolojia kutokana na mwanamke kuwa na woga wakati wa tendo._
_Kuwa na makovu ukeni kutokana na athari za kukeketwa, uwepo wa michubuko na vidonda au maambukizi ukeni mfano fangasi ya muda mrefu na maambukizi mengine hasa magonjwa ya ngono._
_Uvimbe ukeni au uwepo wa jipu na vipele, kuumia kwa kufanyiwa vipimo au baada ya kuzaa kwa njia ya kawaida endapo hukupona vizuri._
Kuhisi maumivu baada ya tendo*
_Maumivu haya hutokea muda mfupi baada ya tendo la ndoa._
_Mwanamke huhisi maumivu kwa ndani zaidi ukeni au chini ya tumbo._
_Maumivu huwa makali na huchukua muda mrefu._
_Maumivu ya chini na ndani zaidi ukeni huleta hisia kama muwasho mkali wa pilipili au kama unakatwakatwa na viwembe na ukinawa unazidi kupata maumivu._
_Maumivu ya ndani zaidi ukeni wakati mwingine huambatana na hali ya kuhisi kama kuna kitu kinasukumwa wakati wa tendo na unapomaliza tendo ukinawa unahisi kitu kimevimba ndani ukeni kama kigololi._
_Maumivu huwa chini ya tumbo na wakati mwingine husambaa kulia na kushoto ya mirija._
_Wengine huumwa na kiuno hata kutembea inakuwa shida mara tu baada ya kumaliza tendo._
_Hali ikiwa mbaya mwanamke hutokwa na damu baada ya tendo, hali ambayo siyo dalili nzuri kwani hata saratani ya shingo ya uzazi nayo huonyesha dalili hii ya damu._
_Hali ya maumivu pia huambatana na kutokwa na majimaji ukeni wakati mwingine yakiambatana na muwasho mkali na harufu._
_Hata wanaume wanaweza kutokwa na damu baada ya tendo badala ya manii._
Nini cha kufanya?*
_Tatizo hili ni kubwa na lina vyanzo vingi kama tulivyoona, hivyo ni vema kufanya uchunguzi kujua chanzo halisi ndiyo tiba ifuate._
_Epuka kutumia dawa bila ya kujua chanzo halisi._
_Uchunguzi hufanyika katika hospitali no vema
No comments: