Mke wangu ananipiga makofi kila ninapochelewa kurudi nyumbani, nifanyaje jamani nimechoka!.

Image result for mwamke

Mimi ni mwanaume niliejaaliwa kuwa na watoto wawili wakike na wa kiume na mke wangu nimemuoa miaka kumi iliyopita huko mkoani iringa, shughuli zangu ni fundi seremala katika hizi kampuni za ujenzi za kichina zilizotapakaa hapa jijini dar ambazo tunajenga nyumba mbalimbali za miradi ya jamii.

Sasa mara nyingi pesa huwa tunalipwa kwa kila wiki, sasa hapa kati huwa napigika sana yaani nakuwa sina pesa hivyo ni lazima nijiongeze kwa kufanya kazi za ziada pindi ninapotoka kazini ile saa kumi, sasa najikuta nakuwa huko mitaani mpaka saa mbili au saa tatu usiku ndipo namaliza kazi zangu za ziada na kupata pesa then naelekea home.

Lakini ninapofika nyumbani nakumgongea mke wangu anifungulie mlango nikiingia ndani tu maneno yanaanza, nikimjibu kuwa nilipitia sehemu kufanya kazi maana nimerudi kazini nikiwa sina pesa naambulia vibao usoni napigwa mpaka nalia ndugu zangu huku nikiambiwa na mke wangu...usinijibu mimi nakwambia...roho inaniuma sana ndugu zangu naomba  nifanye nini ili kuepukana na vipigo hivi mimi jamani?.

No comments:

Powered by Blogger.