Punyeto ni nini na nini madhara yake?

Image result for madhara ya kupiga pull


Kufanya au kupiga punyeto, ni tendo la kutomasa sehemu zako mwenyewe za siri ili kujisisimua kimapenzi.

Kwa hivyo katika kupiga punyeto hamna hofu ya kuambukizwa magonjwa yanayosambazwa kupitia ngono, kwani haimshirikishi mtu mwengine.

Punyeto ni toshelezo kamili la kimapenzi kama utatumia njia mbali mbali za kujitomosa na kujipa papasa ya kujistarehesha.

Hakuna mtu anayezaliwa akijua jinsi mwili wake unavyoitikia msisimko wa kimapenzi. Inakubidi kujifunza kwa majaribio salama.

Na, kwa vile kila mtu yuko tofauti, njia nyengine ya kujua jinsi unavyoweza kumstarehesha mpenzi wako, ni kujifunza kutoka kwako mwenyewe.

Shughulika zaidi na sehemu ambazo zinasisimka kwa urahisi.

Unaweza kufikia kilele cha starehe yako kwa kuitomasa tomasa mboo au kisimi, lakini kutakupa hamu kubwa na ashiki, na kufikia kutoshelezwa vya kutosha, kama utapapasa pia sehemu nyenginezo za mwili wako.

Kwa nini punyeto huonekana kuwa makosa?

Msimamo wa dini nyingi na watu wengi ni kuwa punyeto ni dhambi, mwiko, jambo lililokatazwa, jambo lisilokubalika kabisa.

Lakini wanasanyansi wanasema ni jambo salama kiafya na dhana zilizopo kulihusu, ni imani za kibinafsi na chaguo la mtu.

Wanaume wengi na wanawake hupiga punyeto maishani mwao, kwa sababu huwafanya wakajisikia vizuri na huondoa dhiki za mihemko ya kimapenzi bila kujiingiza katika ngono na mtu mwengine.

Pia hofu ya kuambukizwa magonjwa ya zinaa, ikiwemo virusi vya HIV ni kichocheo tosha kinachopelekea baadhi ya watu kupiga punyeto. 

Lakini kuna sehemu wanaeleza hivi:

Punyeto (kujitoa manii kwa mkono):

"Punyeto" ni: Dhana inayowakilisha tendo la kujitoa/kushusha manii kwa njia isiyo jimai. Kupiga punyeto kwa kutumia kiungo/zana yo yote ile ni tendo la haramu mbele za Mafaqihi walio wengi. Na hiyo ndio kauli ya Mafaqihi wa madhehebu ya Imamu Maalik, Shaafiy na Abu Haniyfah. Lakini uharamu wa punyeto mbele zao uko chini ya uharamu wa zinaa; yaani zinaa ni haramu zaidi kuliko punyeto ingawa vyote ni haramu. Kwa muono wao huu, lau mtu ataangukia katika mtelezo wa kutenda mojawapo ya haramu mbili hizi; zinaa na punyeto. Basi hapana makindano kwamba aegemee zaidi janibu ya punyeto ili kuilinda nafsi yake dhidi ya uchafu wa zinaa. Atafanya hivyo kwa mazingatio ya msingi wa Fiq-hi usemao: "lenye madhara khafifu baina ya yenye madhara mawili" na "lenye shari kidogo baina ya yenye shari mawili".

Ama madhehebu ya Imamu Ahmad na maimamu wengineo-Allah awarehemu-ni kuhalalisha punyeto kwa kuizingatia kuwa ni nyenzo inayoweza kumsaidia muhusika kujikinga na zinaa. Na wala hapa hatukusudii na wala hatuna nafasi ya kutaja mkururo wa dalili za kauli mbili hizi; haramishi ya kundi kubwa na ile halalishi ya kundi dogo. Bali tunalazimika na kutosheka na kuashiria kwamba waliosimamia kauli ya uhalali. Hawakusema hivyo ila ni kwa sababu wameona tendo hili linampa kinga ya kiasi fulani mwanadamu dhidi ya kutenda uchafu na uoza wa zinaa. 

Hili ndilo walilolizingatia na kulijengea kauli yao hii ya uhalali, lakini hapo hapo hawalioni tendo hili kuwa ni halali iwapo litageuzwa kuwa ndio ada/desturi na mazoea ya mtu. Akawa analifanya zoezi hili kwa kuendelea kiasi cha kuifanya punyeto kuwa maradhi ya nafsi/siha. Kwa sababu hakuna hata mwanachuoni mmoja anayehalalisha madhara hata kama hicho chenye kudhuru kilikuwa halali katika asili yake. 

Mathalan tendo la kula, asili yake ni halali na wakati mwingine huwa ni wajibu kwa kiwango cha dharura/ulazima wa kuhifadhi uhai. Lakini tendo hili hili linaweza likawa haramu pale mtu atakapokula zaidi ya uweza/shibe yake na akasababisha kuidhuru nafsi yake. Kwa msingi wa maelezo haya basi, hapana makindano baina ya maulamaa wetu-Allah awarehemu-katika suala zima la kuharamisha punyeto. Kwa sababu tendo hili linaidhuru kano/mishipa ya nguvu ya muendekeza tendo hilo na kulifanya kuwa ndio mchezo wake. 

Kama linavyoudhuru mfumo mzima wa viungo vyake vya uzazi (reproductive system) na afya yake kwa ujumla. Kwa hivyo basi, si Imamu Ahmad wala imamu mwingine anayehalalisha kile kinachosababisha madhara kwa hali yo yote. Kwa mapenzi mema kabisa, tunawasihi na kuwanasihi vijana wetu wa kiume na wale wa kike kutoendekeza zoezi hili la kujitoa manii kwa njia isiyo ya jimai. Tena waache kabisa hata kufikiria kulitenda, kwa sababu tendo hilo ni hatari kwa afya zao.

Mwanachuoni mkubwa; Sheikh Muhammad Al-Haamid-Allah amrehemu-katika kitabu chake {RUDUUDUN ‘ALAL-ABAATWIYL}, ametaja maneno kima kuhusiana na maudhui hii, tunamnukuu: "Hakika tene (kichwa cha dhakari) ina hisia kali sana na hapo ndipo patokapo hisia (za raha na ladha) wakati wa tendo la jimai kwenda kwenye kifuko cha manii (spermatic vesicle). Na kusababisha kijibinye ili kitoke humo kiasi fulani cha manii na kuchanganyika na kitu kinachoitwa "prostate gland". Na hapo katika mchanganyo huo ndipo huundika mmiminiko maji huu ambao kutoka kwake huzipoza na kuzituliza shahawa/ashiki/matamanio. 

Sasa basi mtu atakapodumu na zoezi la kuichezea dhakari yake, ngozi ya tene huwa ngumu na kusababisha kudhoofika kwa nguvu-hisia zake. Na kuyafanya manii kutoka bila ya kuchanganyika na ute wa "prostate" ambao una athari na mchango mkubwa katika kutuliza kiamshi-shahawa. Kwa hivyo basi manii yanapokuwa hayakuchanganyika na ute huo, kupoa kwa shahawa huwa ni kwa muda mfupi tu, kisha huamka tena kwa nguvu kubwa. 

Kwa ajili hii humlazimisha mpiga punyeto kupiga tema mara ya pili, tatu.... na kama hivi. Mpaka mwishowe humwaga damu (badala ya manii), kwa sababu ya kumaliza kabisa kile kiitwacho "spermatic cord/funiculus" na kuudhoofisha kwake mfumo-uzazi kutokana na wingi wa kupiga punyeto. Kinachotokea kutokana na udhaifu wa hisia wa tene kwa sababu ya wingi wa kupiga punyeto: Ni kwamba mwenye kuzoea kupiga punyeto, hutokezea akashindwa kufanya jimai kwa namna anayoweza kufanya mtu asiyefanya mchezo huo. Hii ni kwa sababu tene iliyodhoofika kutokana na wingi wa kupiga punyeto haiathiriki (na tendo la jimai) kwa kiwango kihitajiwacho kutokana na msuguano ndani ya uke. Kwa hivyo basi hawezi kushusha manii ila kwa kujichua na mkono. 

Ndani ya tendo hilo kuna madhara kwa nafsi yake na mkewe ambaye ana haki ya kutoshelezwa nae (ili asifikirie/kufanya machafu) kwa jimai halali". Mwisho wa kumnukuu sheikh-Allah amrehemu.

Kwa kuungia maneno kima haya ya sheikh tunaongezea: Kwamba manii ni kimiminika muhimu mno cha mwili na mfumo mzima wa uzazi. Chini ya maana hii Muingereza Dr. Mary Stoubis anasema katika kitabu chake {MARRIED LOVE}: "Kwa yakini mchanganuo wa kikemia wa kimiminika hiki manii, umedhihirisha kwamba pamoja na vitu vingine unahodhi kiwango kikubwa cha "phosphoric acid" na "calcic acid". Na zote mbili hizi ni maada kima zenye taathira adhimu katika ujenzi wetu wa kimwili (kama wanadamu). 

Hili likisihi (kuwa sahihi), basi kwa hakika kosa kubwa analolifanya mwanadamu ni kudhania kuwa maada manii ni kitu ambacho kunasihi kujitakasa nacho baina ya kipindi kifupi na kingine. Na kuimwaga hovyo bila ya malengo na kuona haja ya kuihifadhi".

Ni mazuri yaliyoje maneno ya mshairi huyu anayesema na vijana:

{Yahifadhi manii yako kiasi uwezavyo kwani hayo *** Ni maji ya uhai yamwagwayo katika matumbo ya uzazi}.

No comments:

Powered by Blogger.