TAMBUA LIMBWATA KALI LA PAKA NA MADHARA YAKE
Limbwata la paka ni ulozi ama uchawi wa mapenzi anao fanyiwa mtu kwa lengo la kumfanya aliefanyiwa uchawi huo amn’gan’ganie na kumganda mtu alie fanya uchawi huo.
Mara nyingi uchawi huu hufanywa na wapenzi wanao ishi pamoja au wapenzi wenye tabia ya kula chakula kwa pamoja au mpenzi anae weza kumpikia chakula mpenzi wake.
Ni uchawi unao fanya kazi kwa watu ambao tayari wapo katika mahusiano ya kimapenzi na wanashiriki tendo la ndoa .
Jinsi limbwata la paka linavyo tengenezwa
Sio dhamira yangu kuwafundisha watu ulozi, lakini kwa dhumuni la kujifunza nitaeleza kwa ufupi namna na jinsi limbwata la paka linavyo tengenezwa, japo baadhi ya vitu nitavificha kwa sababu maalumu.
Mahitaji :
Ili wachawi waweze kutengeneza limbwata la paka ni lazima wawe na vitu vifuatavyo :
1. Mti mweupe : Mti huu unapatikana porini, mti huu ukikomaa, urefu wake hauzidi wa mtoto wa miaka saba, una magamba kwa mbali na rangi yake ni nyeupe.
Mti huu ukikauka ukausaga unga wake huwa mweupe kama mti wenyewe.
Ukichukua unga wa mti huu halafu ukajipaka usoni unakuwa na uwezo wa kuwaona wachawi.
Ukijipaka unga wa mti huu usoni halafu ukatembea mtaani wakati wa mchana, unaweza kuona mambo yote yanayofanyika katika siri kubwa kama vile wachawi wakiwa wanawanga au wanafanya shughuli zao wakiwa uchi.
Dawa hii itakupa pia uwezo wa kuwaona misukule.
Vilevile mti huu una uwezo wa kukimbiza nyoka mfano ukiwa na kipande cha mti huu mfukoni halafu ukawa unatembea, kama mbele yako kuna nyoka atakimbia kabla hujafika.
Hata ukikaa mahali kama kuna nyoka hawezi kukaa hapo, atakimbia tu.
2. Mpapatiko : Huu ni mti wa porini wenye matumizi mengi sana katika utabibu
3. Namata : Huu ni mti wa porini wenye kutoa matunda yanayo nasa kwenye nguo. Ukipita porini au kwenye vichaka mahali ambako huu mti unapatikana basi matunda ya mti huu yatanasa kwenye nguo zako.
4. Mizizi ya msada
5. Mizizi ya mbaazi
6. Kipande cha mti ulio chukuliwa kwenye fimbo za kwenye kitanda cha sokwe mtu.
7. Mifupa ya samaki alieliwa na mtu aliekusudiwa kufanyiwa uchawi huu
8. Au mifupa ya nyama ya ng’ombe iliyo liwa na mtu aliekusudiwa kufanyiwa uchawi huu
9. Utumbo wa mbuzi
10. Damu ya hedhi ambayo imetoka wakati mwanamke akiwa usingizini
11. Dume na jike la njiwa ambayo yamezaliwa pamoja
12. Paka mweusi
13. Kasuku
14. Gamba alilo jivua nyoka
15. Chura mkubwa alie kaushwa pamoja na minyoo. Hii minyoo inakuwa imemfunga chura na anakaushwa nayo akiwa hai.
16. Gamba alilo jivua nyoka
17. Ini la samaki mmoja wa baharini
18. Kinyonga alien’gan’gania mkia wake kwenye mti wakati anazaa.
19. Uzi au nguo aliyo ivaa mkusudiwa
20. Manii za aliekusudiwa
21. Chumvi ya mawe punje ishirini na moja
22. Njugu mawe punje ishirini na moja
23. Talasimu saba za kichawi
24. Pamoja na aina nyingine tisa ya miti ya porini.
MATAYARISHO
Matayarisho ya ndumba hii huwa kama ifuatavyo :
1. Kupata mifupa ya samaki alie liwa na mtu aliekusudiwa kufanyiwa uchawi au mifupa ya nyama iliyo liwa na mtu aliekusudiwa kufanyiwa uchawi.. Baada ya kupata chakula cha pamoja basi anaekusudia kufanya uchawi huu atakusanya mifupa yote kutoka kwenye samaki au nyama aliyo kula mhusika. ..Isiwe kutoka kwenye kuku wa kizungu. Kama ni kuku basi awe kuku wa kienyeji… Mifupa hii itahifadhiwa kwenye kitambaa au mfuko.
2. Kupata manii za mwanaume alie kusudiwa: Baada ya kumaliza kufanya mapenzi, basi itachukuliwa kondomu ambayo ndani yake kuna manii za mwanaume alie kusudiwa na kama watakuwa wamekutana bila kutumia kondomu basi mwanamke atajifuta kwa kitambaa na kukihifadhi kwenye mfuko.
3. Kuunganisha damu ya paka na nafsi ya mwanaume alie kusudiwa : Lengo la zoezi hili ni kuunganisha nafsi au damu ya mwanaume alie kusudiwa kufanyiwa uchawi huu na nafsi ya paka ili kumfanya mwanaume huyo kuwa na “ hadhi “ ya paka katika ulimwengu wa rohoni.
Kama nilivyo sema katika makala yangu yaliyo pita, uhai wa mtu yoyote Yule upo kwenye damu yake. Na story ya maisha ya kila mtu imeandikwa kwenye damu yake. Pia nikasema kuwa, damu ya mtu yoyote Yule huwa ina sifa moja kuu , nayo ni chochote utakacho kiunganisha na damu ya mtu basi kinakuwa sehemu ya damu hiyo na kinakuwa ni mtu huyo kabisa. Sasa basi zoezi hili hufanyika kwa lengo la kuunganisha damu ya mwanaume alie kusudiwa na damu ya paka ili kumfanya mwanaume huyo kuwa na hadhi ya paka katika ulimwengu wa rohoni.
Zoezi hili hufanyika saa sita usiku kwenye njia panda jike : Wanachukuliwa njiwa wawili jike na dume walio pasuliwa pamoja , mioyo yao inatolewa inaunguzwa hadi iwe majivu. Damu inawekwa kwenye chungu cheusi .
Anachukuliwa paka mweusi anachinjwa , moyo unatolewa unachanganywa na mioyo ya njiwa na kuunguzwa tena pamoja hadi iwe majivu, damu inachanganywa kwenye chungu.
Halafu baadae anachukuliwa njiwa anachinjwa, moyo unachanganywa kwenye mioyo ya njiwa na paka na kuunguzwa pamoja , damu inachanganywa kwenye chungu.
Chungu kinakuwa na damu ya njiwa wawili, damu ya kasuku na damu ya paka, ndani yake zinaongezwa shahawa za mwanaume alie kusudiwa au kitambaa kilicho tumika kumfuta shahawa zake pamoja na unga wa mti mweupe na dawa nyingine za kichawi.
Lengo la kutumia damu ya kasuku hapa ni kwa ajili ya kufungua njia ya kuingia katika malango ya ufalme wa wanyama ili kuunganisha nguvu kati ya damu ya mwanaume alie kusudiwa ( kupitia manii zake ) na damu ya paka.
( Katika ulimwengu wa kiroho, kasuku ndio lango kuu la kumuunganisha mwanadamu na ufalme wa wanyama.. Mnyama mwingine anae tumika kama lango la kuunganisha nguvu kati ya mwanadamu na wanyama ni kunguru )
Damu hizo zitaachwa hadi kesho yake saa saba mchana. Lengo ya kuziacha damu hizo kwenye chungu huku kikiwa wazi ni kwa ajili ya kuzitoa kama sadaka kwa Jua.
Damu hizo hutolewa ili jua liweze “
kunywa” damu hizo.
Kesho yake saa saba mchana watakapo rudi mahali kilipo chungu hicho, watakuta damu imekauka.
Kukauka kwa damu ni ishara kwamba, jua limekubali sadaka hiyo. Jua limekunywa damu hiyo. Sadaka imekubaliwa.
4. Kupika uchawi sasa : Baada ya hapo vitachukuliwa vitu vyote nilivyo viorodhesha hapo juu, vitawekwa pamoja kwenye chungu, vitaunguzwa hadi kuwa majivu. Majivu hayo yatachanganywa na majivu ya mioyo ya njiwa, paka na kasuku. Ndumba hiyo itakuwa tayari kwa matumizi.
Jinsi limbwata hili linavyo tumika :
Itachukuliwa dawa hiyo, mrogaji ataenda sehemu ambayo kunapatikana huduma ya chakula na paka wengi, kama vile kwenye bar.
Akifika hapo ataagizia nyama. Paka watamsogelea kumzonga ili awarushe kipande cha nyama. Atachukua kipande cha nyama isiyo na mfupa, atakiweka mdomoni kipate mate mate yake kisha atakakipaka hiyo dawa halafu atamrushia paka ale. Paka akisha kula basi huyo mwanaume alie tengenezewa inakuwa ni kwisha habari yake.
Madhara ya Limbwata la Paka kwa alie fanyiwa
Uchawi huu huwa na madhara makubwa sana kwa alie fanyiwa. Baadhi ya madhara hayo ni kama ifuatavyo :
i. Atakuwa anakufuata kila mahali. Kama ni mke na mume mnaishi nyumba pamoja basi kila sehemu hapo nyumbani atakuwa anataka kuwa na wewe. Sebuleni, jikoni,bafuni nakadhalika.
ii. Atakufuata na kun’gan’gania kuwa na wewe muda wote kila mahali kuanzia sokoni, nyumba ya ibada, vikoba n.k.
iii. Kama ni muajiriwa basi atakuwa anatoroka kazini kuja kuonana na wewe mahali popote utakapo kuwa.
iv. Kama ni mfanyabiashara atakuwa anatoka kwenye biashara yake anataka kuja kushinda na wewe.
v. Hata ukimfukuza yeye atakuwa yupo na wewe tu kama paka anae fukuzwa na mtu anaekula nyama.
vi. Matokeo yake sasa : kama ni kazi, atafukuzwa kwa sababu lazima ataharibu tu ofisini
vii. Na kama ni biashara basi biashara yake itakufa kabisa kwa sababu muda mwingi atakuwa na wewe.
viii. Atakuwa kama zoba, ndondocha au zezeta.
ix. Ni vigumu sana kumrudisha katika hali yake ya kawaida na akirudi katika hali yake ya kawaida basi anakuwa kama mwendawazimu na maisha yake hufeli kabisa.
x. Na mwisho wa siku watu walio fanyiwa uchawi wa namna hii hua wanasalia kuwa walio changanyikiwa na kibaya kuliko zote familia hukosa maendeleo kwa sababu baba ndio kichwa cha familia na ameshatiwa uchizi,kiasi hawezi kutafuta tena.
JINSI YA KUMZINDUA MWANAUME AU MWANAMKE ALIE LISHWA LIMBWATA LA PAKA .
Mwanaume au mwanamke aliyelishwa kwa limbwata la paka anaweza kuzinduliwa kwa kutumia dawa inaitwa
Mwavi almaarufu kama Kishinda wachawi. Mwavi ni mti ambao kwa hapa Tanzania unapatikana Kigoma tu , na katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na kati mti huu unapatikana Kigoma na Congo Mashariki sehemu inajulikana kama Moba.
Ni dawa inayo ua uchawi wa kila aina. Inaweza kutumika kwa kuoga au kunywa kulingana na mahitaji ya mgonjwa. Na kama afya ya mgonjwa ni dhaifu ama anasumbuliwa na maradhi makubwa kama vile kisukari au presha basi haruhusiwi kutumia dawa hii kwa kunywa kwa sababu ina nguvu sana…Unaweza kujaribu kuipata dawa hii kwenye maduka ya dawa za asili lakini kwa uhakika kabisa nenda Kigoma, huko utaipata bila wasiwasi
No comments: