Tatizo la uke kuwa mkavu,chanzo na matibabu

Image result for matatizo ya uke mkavu


Kwa kawaida kwa kila 
uke wake unapaswa kuwa na hali ya unyevunyevu kutokana na ute mwepesi unaozalishwa ili kusaidia kuuweka uke katika hali hii.
Hormone inayojulikana kama estrogen ndo inayofanya kazi ya kufanya ute ute huu kuzalishwa ili kufanya uke kuwa na unyevunyevu na kuta za uke kuwa zinavutika(elastic).Pia ute huu husaidia kuweka sawa mazingira rafiki kwa mbegu za kiume,ili zinapokuwa zimeingia zisiweze kufa hadi zinapolifikia yai.

Kushuka kwa kiwango cha hormone ya estrogeni ni chanzo kikubwa cha kupungua kwa ute huu na kufanya uke kuwa mkavu.Kiwango cha hormone kinaweza kushuka kutokana na sababu mbali mbali kama tutavyoona katika makala hii.

Inaweza kuonekana ni jambo dogo,lakini kutokua na unyevunyevu wa kutosha inaweza kuathiri maisha ya muhusika haswa katika swala la kujamiiana.Ikiwemo kusababisha tatizo la maumivu wakati wa tendo la ndoa, na kupata tatizo la fangasi za ukeni mara kwa mara

CHANZO CHA TATIZO
Tatizo la uke kuwa mkavu linawakumba sana watu waliofikia ukomo wa hedhi (Menopause) Kutokana na sababu kwamba mwanamke anapofikia kipindi hiki mwili unapunguza au kuacha kutengeneza hormone hii ya estrogen. Hali hii hupelekea kuta za uke kuwa nyembamba na hazivutiki tena hali ambayo kitaalamu inajulikana kama Vaginal Atrophy.

Kiwango cha estrogen kinaweza pia kushuka kutokana na vitu vifatavyo:

1.Kuzaa na kunyonyesha. Kipindi hiki mwili unazalisha hormone ya maziwa (prolactin hormone) ambayo pia inazuia kuzalishwa kwa hormone ya estrogen.
2.Matibabu ya saratani. (Tiba ya mionzi na dawa za saratani)
3.Kutolewa mifuko ya mayai( ovaries)
4.Dawa zinazozuia uzalishwaji wa hormone ya estrogen kwa watu wenye tatizo la Uvimbe kwenye kizazi, (fibroids na endometriosis)

SABABU NYINGINE ZA UKE KUWA MKAVU NI: 
SJOGREN SYNDROME ,Huu ni ugonjwa ambao kinga ya mwili inaharibu cell zinazotengeneza huu unyevunyevu
Dawa kutibu mzio( allergy) na mafua
Kusafisha uke hadi kwa ndani (douching)
Kusafisha uke kwa kutumia sabuni zenye kemikali
Kutoandaana kabla ya kufanya ngono.

UCHUNGUZI
Unapopata muwasho,au maumivu wakati wa tendo la ndoa na kuona uke wako ni mkavu vyema ukafika hospitali au ukawasiliana na daktari.Daktari atakuuliza maswali muhimu ili kubaini chanzo cha tatizo na atakufanyia vipimo na uchunguzi na atajua dawa gani inafaa.

MATIBABU
Matibabu yaliyozoeleka katika hili tatizo la ukavu ukeni ni kwa kutumia Estrogeni za kupaka au kupachika ukeni (topical estrogen),
Pia estrogen inaweza kuwa kaitka miundo mbali mbali kama ifatavyo:

Ring (estring) Hii inakua ni kitu cha duara kama pete ambacho mtu anawekewa ukeni,kinakua kinazalisha hormone ya estrogen,na kinabadilishwa kila baada ya miezi mitatu

Vidonge (Vagifem),Vidonge hivi ni bya kupachika ukeni vinakua na kifaa chake maalumu cha kusaidia kuviingiza ukeni.Unapachika kidonge kimoja kwa siku ndani ya muda wa week mbili.

Dawa za kupaka /cream (Estrace na Prematin)
Dawa hizi unapaka ukeni kila siku kwa muda wa wiki mbili.

MUHIMU: Dawa zenye Estrogen zinakuwa na maudhi madogo madogo (side effects) kama matiti kuvimba na kuuma na dawa za estrogen hazipaswi kutumiwa na watu wenye matatizo yafuatayo:
Saratani ya matiti
saratani ya shingo ya kizazi
Wajawazito na wanonyonyesha


TATIZO LA UKE KUWA MKAVU | CHANZO NA MATIBABU - 0765203999

No comments:

Powered by Blogger.