Wanawake: Tatizo la Kutokwa na Uchafu Ukeni na jinsi ya kukabiliana nalo
Kimsingi wanawake wote hutokwa na uchafu kidogo ukeni ambao ni mweusi kama maji, maziwa au njano ambao humfanya ama awashe au atowe harufu mbaya pale anaposhindwa kukabiliana na hali ya usafi wake. Hata hivyo, wanawake wengi kipindi cha ujauzito hukumbwa na hali hii mara kwa mara na huwashwa. Uchafu husababishwa na mambo mbalimbali ambapo mengi husumbua japo si hatari. Zifuatazo ni aina za uchafu ambao wengi huwakumba na jinsi unavyoweza kukabiliana na tatizo hilo.
Mwanamke aliye na tatizo la kutokwa na aina hii ya uchafu hujikuta ananuka na kujikuna sehemu zake za siri, na huu unawezekana kuwa ni ugongwa wa Trichomos kwani pindi anaposikia haja ndogo hujisikia kuchomwa sana na maumivu ambapo wakati mwingine hujikuta anavimba.
Uchafu wa aina hii huonekana kama picha kushoto inavyoonyesha hivyo mwanamke ambaye atakumbwa na tatizo kama hili ni rahisi kumfanya mpenzi wake apoteze hamu ya kushiriki naye tendo la ndoa na kama ni mpenzi basi huweza kujikuta kila kukicha anashindwa kudumu na mwanaume kwani hukimbiwa kutokana na kushindwa kwao kukabiriana na tatizo hilo.
Endapo una tatizo hili ni muhimu sana kuhakikisha unaweka viungo vya uke wako katika hali ya usafi wa kutosha, na ni vema unaposafisha uke wako uhakikishe unatumia maji ya uvuguvugu pamoja na siki au maji la limao yaliyochanganywa na maji ambapo unapaswa kutumia vijiko 3 vya siki kwenye maji lita moja yaliyochemshwa. Ni muhimu mgojwa asafishe uke wake mara moja hadi tatu kila siku mpaka apone!
Hata hivyi endapo tatizo hilo linakuwa kubwa, mgonjwa anapaswa kutumia dawa za kuchomeka ukeni ambazo zina metronidazole au dawa zingine zinazoshauriwa na trichomonas. Ikiwa hali mbaya sana anapaswa kumeza metronidazole kwa kiasi cha gram mbili [meza kwa mpigo].
Aidha, inawezekana kuwa mwanaume ana ugonjwa pia wa trichomonas ingawa hajisikii hali ya kuumwa hata kidogo hivyo endaapo mwanamke atarudiwa na ugonjwa huu mara baad a ya kujitibu basi anapaswa kurudia kumeza gram mbili za metronidazole, lakini ni kama ugonjwa huo mkubwa.
Hali hii inapojitokeza kwa mwanamke hujikuta anawashwa sana ukeni na midomo ya uke huwa na rangi nyekundu na huuma sana ambapo pindi mhusika napotaka kukojoa husikia maumivu makali sana. Hali hii huwakumba sana wanawake wajawazito pamoja na wale wenye ugonjwa wa kisukari, wale waliokuwa wakitumia antibiotics au vidonge vya kuzuia ujauzito.
Endapo una tatizo hili ni muhimu sana kuhakikisha unaweka viungo vya uke wako katika hali ya usafi wa kutosha, na ni vema unaposafisha uke wako uhakikishe unatumia maji pamoja na sikiau GV vijiko viwili kwa nusu lita au kutumia vidonge viwili vya nystatin vya kuchomeka ukeni au dawa nyingine ya thrush kama siyo kuweka maziwa mgando yaliyochachuka kwenye uke husemakana ni dawa nzuri ya kienyeji inayotibu tatizo hili.
No comments: