Jinsi Ya Kumdhaifisha Mwanamke Ili Akupende

Ikija katika maswala ya udhaifu katika mwanamke, huwa kuna baadhi ya mambo ambayo huwa tofauti katika kila mwanamke.


Hebu mwanzo tuanze kwa kusema kuwa kila mwanamke yuko tofauti. Si kila mwanamke anataka kitu kimoja kwa kila mwanaume. Lakini, kuna baadhi ya mambo ambayo huwa yanajitokeza juu zaidi katika udhaifu wa mwanamke. Kama mwanaume atafanya mambo vile ambavyo inahitajika, basi itakuwa vigumu kwa mwanamke kuukwepa mtego.

Mambo ambayo haswa huwafanya wanawake kuvutiwa na wanaume huwa ni tabia flani ambazo hujitokeza. Hii ni kumaanisha kuwa kila mwanamke huwa amemakinika zaidi kwa mambo ambayo mwanaume hufanya tofauti na sura yake.

Wakati unapotongoza mwanamke lazima ujenge connection ya kihisia zaidi. Hii ni kwa sababu kujenga muungano wa kihisia na mwanamke hudumu zaidi ukilinganisha na umbo lako. Kile kitu ambacho unahitaji zaidi katika mahusiano yako ni kuwa na muungano wa kihisia.

Kama kweli unataka kumvutia mwanamke, unahitaji kuwa mdhaifu wake. Kama atashindwa kujizuia na kuvutiwa kwako, basi utakuwa na nafasi rahisi ya kuuteka moyo wake. Lakini kwanza, unapaswa kujua ni nini haswa kinachochangia hadi mwanamke kuwa mdhaifu mbele yao. Haya hapa ni mambo ambayo humfanya mwanamke kuwa mdhaifu.

#1 Kuwa mkarimu wa ukweli. Hauwezi kufeki jambo hili. Wanawake kwa kawaida huvutiwa na wanaume ambao wanaonyesha ukarimu wa ukweli. Ukiwa mkarimu kwa wengine, itamuonyesha mwanamke vile ambavyo utamchukulia. Huu ni udhaifu mkuu kwa kila mwanamke.

#2 Tabia za usaidizi. Udhaifu wa kila mwanamke ni kuwa na mwanaume msaidivu. Wakiwa wanapewa sapoti na mtu, huwa kawaida wanavutiwa na mtu kama huyo. Kuna kitu ambacho hujitokeza ndani yako wakati kuna mtu anajitokeza na kukusaidia katika maisha yako. Kwa mwanamke huwa maradufu. Usaidivu wako kwa mwanamke kunamfanya awe dhaifu kwako.

#3 Kushangilia mambo anayotimiza katika maisha yake. Kwa kuongezea usaidivu wako, wanawake hupenda mtu ambaye anafurahia na kushangilia mambo ambayo anatimiza maishani mwake. Wakati wamepandishwa cheo kazini ama amemaliza kufanya mradi wake, kukiwa na mtu karibu yake ambaye atashangilia mafanikio yake kila wakati ni jambo ambalo kila mwanamke anatamani.

#4  Kupendezwa na hamu zake. Hii haimaanishi kuwa udhaifu wa kila mwanamke ni kuiga kila kitu ambacho anapenda, la. Hii ni ile hatua ambayo unakuwa na interest na mambo muhimu ambayo huyapenda zaidi katika maisha yake. Kwa mfano ukimwona mwanamke anapenda sana mchezo wa magongo ama anapenda kufuatilia maisha wa wasanii aina flani, basi wewe jifunze kucheza mchezo wa magongo na pia uanze kuwatambua wasanii husika. Akiona kuwa unapenda mambo ambayo anapenda utakuwa umemdhaifisha.

Haya ndio mambo muhimu ya kuzingatia kama unataka kumfanya mwanamke adhaifike mbele yako. Kando na mambo hayo manne makuu unapaswa kujihami na mambo haya ambayo yatakufanya uuteke moyo wake:

#1 Lazima uwe mmakinivu na maswala yake ya ndani. Wakati mwingine wanaume huchoshwa kusikia malalamishi ya mwanamke lakini siri kuu ya kumteka mwanamke ni kuwa msikivu kwa kila kitu anachokuambia coz atakuona kama jangina wake wa maisha.

#2 Mpe saport kwa kila kitu. Kuna wakati anaweza kuongea mambo ambayo kwa msingi unaona kuwa hawezi kutimiza. Akifikia hapo wewe unapaswa kunyamaza tu. Unapaswa umpe sapoti kwa kila kitu. Haijalishi kama unamuelewa au la, unapaswa umsaidie tu.  Bora tu mambo yake anayojaribu kutimiza hayamdhuru yeyote ama yeye mwenyewe.

#3 Muulize maswali. Unaweza kuona labda jambo hili halina maana yeyote. Lakini ukiwa unamuuliza maswali mara kwa mara kuhusiana na miradi yake ama mambo anayofanya siku baada ya nyingine utakuja kumuelewa zaidi. Hii itasaidia kwa sababu atakuona unajihusisha na maswala yale ya maisha hivyo atavutiwa na wewe na utatumia swala hili kama udhaifu wake.

Upo!?

No comments:

Powered by Blogger.