Maswali 33 Ya Kumuuliza Mwanamke Unapokutana Naye Mara Ya Kwanza

So finally umekuwa jasiri ukamuapproach huyu mwanamke na ukajitambulisha ipasavyo. Lakini swali ni, “Je, huyu mwanamke utajuaje kama atakufaa?” Nesi Mapenzi imeandikia maswali ambayo unapaswa umuulize mwanamke ambaye umekutana naye kwa mara ya kwanza.

Kwa kawaida huwa ni furaha ya ajabu kukutana na watu wapya katika maisha yako. Haswa wanawake warembo ambao unapangia kuwadeti ama labda kuwaoa siku moja katika maisha yako.

Lakini katika harakati ya kuzungumza na mwanamke huyu, unaweza kumbwa na changamoto ya maswali. Si kila mwanaume ana uwezo wa kumuuliza maswali yafaayo kwa mwanamke, so hapa ndio tumeingilia kati.

Maswali muhimu ya kumuuliza mwanamke ambaye umekutana naye mara ya kwanza.

#1 Umetoka wapi? Swali hili liko moja kwa moja na ni ibada kuuliza mwanamke yeyote.

#2 Unafanya nini kujimudu? Swali hili utapata kujua mambo ambayo anapenda na ni vitu gani angependa kuchangia katika dunia ya sasa.

#3 Kitu gani kinakufanya upende kazi yako? Watu wengi huchukia kazi wanazofanya na wanapenda kulalamika. So yeye anamtizamo hasi ama chanya kuihusu?

#4 Wewe unachambua kama mtu wa kuongea sana ama mkimya? Kama wewe ni mtu wa kuparty na yeye ni wa vitabu basi hamtaingiliana.

#5 Ndoto yako ni gani? Muulize angalau kama anaota ama haoti.

#6 Una ndugu? Hapa itakupa nafasi ya kuivamia hulka yake na kujua yeye ni wa ngapi katika familia.

#7 Je uko karibu na wazazi wako? Inaweza kuzua mtafaruku kama hashughuliki sana na wazazi wake, lakini sababu zinaweza kuwa tofauti tofauti.

#8 Unapenda chakula gani? Utatambua tabia yake kulingana na chakula anachopenda.

#9 Unapenda kufanya mambo gani kujiburudisha? Kama wewe unapenda kupiga mbizi baharini na yeye ni mwoga wa hata kupanda gorofa...inaweza kuwa vigumu kwako.

#10 Wapenda concerts? Swali hili litakupa mtizamo wa kujua nyimbo anazopenda, ama labda hata concerts si mambo yake.

#11 Kama ungepewa nafasi ya kubadilisha mwili wako na mtu mwengine katika hii dunia ungemchagua nani na kwa nini? Hii inakupa nafasi ya kutambua kama anajipenda au la.

#12 Mara ya kwanza uliponiona ulinichukuliaje? Hii itakupa nafasi ya kujua iwapo unaweza kuwa na angalau nafasi kwake.

#13 Ni kitu gani unaangalia kwa mwanaume unayepania kudeti? Hapa unapaswa kujitoa, yaani usimuulize direct kama unamaanisha wewe.

#14 Uhusiano wako mrefu ulikuwa upi? Kama unataka tu umeet na huyu mwanamke kwa muda na wala si mahusiano marefu basi utatambua na hapa.

#15 Ni kitu gani romantic zaidi mbacho ulifanyiwa na mtu kwako? Makinika na jibu hili ili wakati mwingine umpe saprize zaidi ya aliyokutajia.

#16 Ni kitu gani zaidi cha kuburudisha katika huu mji? Kama wewe si mkaazi wa huo mji, utapata ideas ya jinsi ya kumfurahisha wakati unapomtoa out.

#17 Kama ungeweza kuishi sehemu yeyote katika hii dunia ungetamani kuishi wapi na kwa nini? Na kama sivyo, kwanini unataka kubaki uliko?

#18 Ungetamani kuwa maarufu? Hapa utajua kama anapenda atenshen ama ni mtu asiyependa kujionyesha.

#19 Kama unataka kuwa maarufu, ni kitu gani ambacho ungetaka kujulikana nacho? Hapa atajieleza na utaijua hulka na mambo anayopenda kufanya.

#20 Mtu gani unayempenda zaidi? Watu wengi hupenda kusema wazazi wao. Lakini labda anaweza kuja na ubunifu zaidi.

#21 Kama ungepata kula mankuli na mtu yeyote – ambaye yuko hai ama amefariki- ungemchagua nani na kwa nini? Hapa majibu ni mengi yatakayotoka kwa kinywa chake. So kuwa tayari kwa jibu lolote.

#22 Uko na rafiki wa dhati? Kama ana marafiki wachache ama wengi utatambua hulka yake.

#23 Una miaka mingapi? Makinika hapa haswa kwa mwanamke ambaye amekupita kimiaka.

#24 Birthday yako ni lini? Hii ni bora zaidi.

#25 Una hobbies zozote? 

#26 Ni mtu yupi ana ushawishi zaidi kwako? Ni muhimu zaidi kumuuliza ni kwa nini na kivipi huyu mtu amemshawishi.

#27 Unatafuta kuingia katika relationship? Hili swali ni muhimu kwa kuwa wakati mwingi unaweza kuapproach mwanamke akakwambia anataka relationship ilhali wewe ni kujirusha naye tu.

#28 Kama umeshinda mamilioni katika mchezo wa bahati nasibu ungezifanyia nini? Atazitumia kulisha maskini ama kuzispend kwa party na magari.

#29 Kama angepewa aombe vitu vyovyote vitatu angechangua nini? Hapa utajua kitu ambacho anakosa katika maisha yake.

#30 Kama umekwama katika jangwa, ni vitu gani vitatu ungehitaji? Hapa utajua huyu ni mtu wa aina gani haswa.

#31 Je kuna msanii unayemzimia? Hungetaka kujua hili haswa tukizingatia siku moja amekufungulia moyo wake.

#32 Unapenda kusoma? Kama ni mtu mjanja kimasomo  ama ni mtu wa kuchukia vitabu tu.

#33 Je unamuamini Mungu? Watu wengi wanahepa kuuliza swali kama hili lakini ni muhimu kwa kuwa utapata nafasi ya kumjua kama unayemtongoza ni mtu wa dini ama ni feki.

No comments:

Powered by Blogger.