Pillow talk - Maongezi nane ya kitandani ambayo yatamfanya akupende sana

Pillow Talk ni kitu gani na ni jinsi gani ya kufanya haya maongezi kuwa mazuri?

Inasemekana kwamba maongezi ya kitandani hufanya maisha ya mapenzi kuwa mazuri zaidi. Lakini Pillow Talk ni kitu gani? Fahamu kila kitu kuhusu pillow talk na jinsi ya kuifanya vizuri.

Kuna mambo mengi sana ambayo yanaweza kufanya uhusiano wa kimapenzi kuwa mzuri.

Kuna miongozo na kuna mitazamo.

Na kuna mambo mengi ya kujifunza na kumbukumbu nzuri za kukumbuka katika mapenzi.


Mawasiliano ni kitu kizuri katika katika mahusiano, lakini kuupata muda mzuri wa mawasiliano ambao utawafurahisha na kuwa mzuri kwa wote wawili huwa ni mgumu kidogo.
Na hapa ndipo Pillow Talk Inapochukua nafasi yake katika mapenzi!

Pillow Talk ni kitu gani hasa?

Pillow Talk ni aina ya 
maongezi unayokuwa nayo wewe na mpenzi wakowakati mmelala wote kitandani.
Na tofauti na mitazamo hasi ya wengi, Pillow Talk siyo lazima ihusishe mada ya kimapenzi au kushikana na mpenzi wako ukiwa kitandani.

Hukuwahi kuwa pamoja na mpenzi wako kitandani na mkawa mnaongelea mada nyingine labda ya maisha yenu, au matatizo sehemu za kazi, au biashara zenu? Ni vizuri unavyokuwa unasikilizana na mwenzio mkiwa kitandani, si ndiyo?

Pillow Talks huwaunganish wapenzi kihisia na kimwili pia(physically and emotionally), na huwaleta pamoja sana tena pale ambapo maongezi hayo yameibuka katika muda muafaka.


Kwanini tunahitaji Pillow Talk katika uhusiano wa kimapenzi?
  
Mojawapo ya faida kubwa ni kwamba, maongezi ya kitandani huleta na hujenga mahusiano mazuri baina ya wapenzi. Kuisikiliza sauti nzuri ya upole ya mpenzi wako mkiwa wote kitandano inaweza kumuondolea stress zote alizokuwa nazo mpenzi wako kwa siku nzima.

Inawafanya wote kwa pamoja mtulie na kuwasaidia kuendelea na maongezi bila ya kuwa na mabishano au hasira, na inawapa muda wa kufikiria jambo kwa upole na undani zaidi. Na wakati maongezi haya yanapokuwa ya kiuaminifu zaidi na ya uwazi, hisia nzito za upendo hujaza mioyo yenu na kupendana zaidi.

Pillow talk ni muhimu maana ni muda mzuri unaowaunganisha wote wawili baada ya masumbuko mbalimbali ya kila siku, na maongezi haya hayana usumbufu wa aina yeyote. Mnaweza kuwa mmeshinda wote siku nzima, lakini hiyo unakuwa unakaa na mwenzio kama afiki yako wa kawaida, lakini kitu ambacho mnahitaji ni dakika chache za kutafakari siku ilivyokwenda ili kujisikia kama wapenzi na sio marafiki au mchepuko.

Kuna wapenzi wenye Pillow Talk, na wapo ambao hawafanyi. Wapenzi ambao hawalali husiku wapo lakini hii haileti furaha kama couple ambayo inafanya pillow talk. 


Mambo ya kuongelea mkiwa kitandani

Je wewe na mpenzi wako ni waongeaji wazuri kabla hamjalala? Kama ilivyo katika maisha, kuna mambo mazuri na mabaya ya kuongelea kitandani. Baadhi ya maongezi yanaweza kukufanya wewe ujisikie upo juu sana katika hii dunia, wakati maongezi mengine yanaweza kukumaliza nguvu na kujisikia kuharibiwa siku kabisa.


Kabla hatujaanza kuongelea maongezi mazuri ya kitandani, ngoja nikupe tips kidogo za maongezi mabaya ambayo unapaswa kuyakwepa au kuyazuia.

Usiongelee matatizo ya maisha yako * labda uwe na utatuzi sahihi wa jambo/ tatizo hilo*. Usiongelee matatizo yako ya kiuchumi, huzuni yako, jinsi ambavyo unavyoonewa, au madhaifu yako ya kazini.

Wapenzi wote huongelea haya mambo, lakini hayo siyo maongezi sahihi ya kitandani. Jaribu kuyachukulia maongezi ya kitandani kama sehemu nzuri na yakiwerevu katika maisha yako. Kama wewe na mwenzio mtaongelea jinsi mnavyoonewa na dunia hii mtalala kwa mawazo lakini pia mtaamka asubuhi mmechoka kama vile mmetoka kulima.

Badala yake, ongelea mambo mazuri, yenye furaha, ambayo yalikufurahisha mchana, yaliyokutamanisha, na kitu kingine chochote ambacho kinaweza kuleta tabasamu katika nyuso zenu. Muwe na ndoto ya maisha ya furaha, na muwe na ndoto ya aina hiyo kwa pamoja. Kama mtakuwa na maongezi ya furaha namna hiyo mkiwa pamoja, yatawafanya mjitahidi sana wakati wa mchana ili kuifikia ndoto yenu.


Aina 8 za maongezi ya kitandani ambayo ni amaizing!

#1. Kufananisha. Hii inaweza kukushangaza, lakini kama binadamu, hupenda kujifananisha na wengine kama tunataka kufurahia kuhusu sisi wenyewe. Yalinganishe mahusiano yenu ya mapezi na mahusiano ya kimapenzi ya marafiki zenu wa chuo au kazini.
Wote mtajisikia furaha kama mahusiano yenu ni mazuri zaidi ya wengine. Na kama kuna kitu mnakitamani kutoka kwenye uhusiano wa wenzenu, wote kwa pamoja mtajikuta mnafana mabadiliko ili kuimarisha maisha yenu ya kimapenzi. 


#2. Ndoto za baadae. Ongeleeni kuhusu matarajio yenu na ndoto zenu katika maisha. Maongezi ya aina hii huwafanya kuzijua ndoto za mwenzako na matarajio yake ya baadae na ni jinsi gani mnaweza kusaidiana ili kuyafikia malengo yenu. Hii inawafanya muwe karibu zaidi.

#3. Pendekeza. Jitahidi kuwa mbunifu kidogo bhanaa. Au tunasema toa comment. Kama asubuhi aliondoka akiwa na nywele salu salu mwambie, lakini kama alipendeza mbwambie. Hii itawafanya wote mtabasamu.

#4. Vitu vipya vya kujaribu wakati ujao. Usifikiri huu ni mda wa kuwaza mambo magumu katika maisha kama nlivyokuambia hapo awali. Badala yake kama kuna changamoto pendekeza njia sahihi inayoweza kulitatua hilo jambo, lakini mambo mapya katika uhusiano wenu kama kwenda honeymoon kwa ajili ya exposure na vitu vingine. Kuongelea mambo ambayo yanalenga kuboresha maisha yenu inafanya maongezi ya kitandani kuwa matamu sana.

#5. Likizo na Exposure. Hakuna kinachofanya maongezi ya kitandani kuwa matamu kama kuongelea na kupanga sehemu za kutembelea baada ya miezi minne ijayo, kwa mapumziko na mpenzi wako au kwa lengo na kubadilisha mazingira na kujifunza(exposure). Jaribu kujadii ni sehemu gani nzuri za kwenda mambo ya kufanya, na mambo mengine mazuri mnayoweza kuyafanya wakati wa likizo. Hii itawafurahisha wote na itawasukuma kujituma zaidi katika maeneo yenu ya kazi na ndoto zenu zitatimia kwa uharaka zaidi.

#6. Kumbukumbu za kimahaba(Romantic Memories). Kuongelea mapenzi yenu ni kitu kizuri kitandani. Muulize mwenzio kama anakumbuka siku ya kwanza alivyokukiss ilikuaje, kama alikua anaogopa mueleze, itamfanya akumbuke mbali na kutabasamu. Maongezi ya aina hii yataanzisha mada nyingine, hivyo hamtapungukiwa na mtajikuta mnajiona wa bahati nyie kuwa pamoja.

#7. Masumbuko ya zamani. Story za zamani ni kama movie inayosisimua na kutia hamasa(inspirational movie), sanasana pale yie wawili mnapokua mnapofanikiwa katia jambo fulani baada ya kusumbuka na kujituma sana. Je, nyie wawili mlihatarisha maisha yenu ili kufanikisha mafanikio ambayo mnayo sasa? Kuyaongelea masumbuko yenu ya zamani na matunda mnayoyachuma sasa hivi inawasaidia kupata takwimu ya mambo mliyofanikiwa na kuwapa kiu ya kufanya mengi zaidi ili kuendelea kuimarika kimaisha.

#8. Ongelea siku yako ilikuaje. Hii aina ya maongezi yanawafanya nyie kuwa karibu katika shughuli zenu za kila siku. Iongelee siku yako, uzuri wako na ubaya wake, ulichofanikiwa na changamoto zilizokukumba na jinsi ya kuzitatua hizo changamoto, na kitu kingine kizuri ambacho kinakufanya ujivuie kwa ile siku kupita.

Kadri mnavyokua mnaambiana kazi zenu za kila siku kwa uwazi, inawafanya nyie mzidi kupendana zaidi na kuwa karibu kimahusiano zaidi kitu ambacho ni vigumu mwingine kuwayumbisha.Itakuwepo nafasi ndogo ya wivu na usaliti, lakini nafasi kubwa ya kuaminiana na kupendana.

No comments:

Powered by Blogger.