Sekunde 7 za maangamizi - Mvutie msichana ndani ya sekunde 7

Je unataka kumpata mwanamke wa ndoto zako? Zifanye sekunde zako 7 tu kumbadilisha kifikra na kumfanya akuone wa thamani!.




Unaweza ukafikiria kitu chochote cha maisha kinachoweza kubadili maisha yako ndani ya sekunde 7? Bila shaka utakua na pressure kubwa sana ndani ya sekunde hizo saba, na wakati mwingine zinaweza kwisha bila kufanya kitu.

Vitu kama kumnunulia mwanamke maua, kumpeleka dinner, kumnunulia chocolates, na vitu vingine vya kimapenzi unazo sekunde saba tu za kumfanya mwanamke afane maamuzi ya kukupa muda wake au la!..

Hapa tutaongelea ni kwa jinsi gai mwanamke anafanya maamuzi ya haraka na ni kitu gani 
utakifanya ili kumvutia kwa mara ya kwanza!
Kwa hiyo ni jambo la awamu - tegemezi

Tuwe wa kweli: Sekunde 7 hazitatosha kumvutia mwanamke. Kama tulivyosema hapo awali: nimkitu gani unaweza kukifana au kukisema ndani ya sekunde 7 ambacho kinaweza kumvutia mwanamke?

Kimsingi hakuna. Badala yake, muonekano huwa ndo kitu kikubwa. Huo ndo ukweli: kama umependeza, hakuna namna yeyote anaweza kukataa kuongea n wewe. Na kama msichana kama kakupa mda uongee naye - nini tena kingine unataka kama sio "kummaliza". Saa nyingine hii haileti picha, lakini kama utashindwa kuwa na mwonekano mzuri(utanashati) hakuna muujiza mwingine unaweza kuutumia. Lakini kuna namna ya kufanya mambo yaende.

Hongera, unaweza kuwa na sekunde 23 zaidi!

Pengine, unaweza kuwa mtu wa kumvutia(interesting person) ambaye hajawahi kuonana naye, pamoja na kuwa na story nzuri za kuvutia ambazo hajawahi kusikia, lakini kama hutaweza kumdaka fikra zake kwa muonekano wako, utakuwa si kitu kwake.

Swali ni kwamba,baada ya kushindwa kushawishi ndani ya sekunde 7 - unawezaje kushawishi kupata sekunde 23 zaidi? Pengine, hii inaweza kuwa bahati, lakini bahati za hivi hutengenezwa! Wale wazoefu wa bar wanajua, ndani ya sekunde 30, mwanamke anaweza kuamua aende kulala na wewe au la!..

Lakini, kiuhalisia hii haimaanishi ndani ya sekunde 30 atakuwa ashakuvulia nguo zake, unaweza tena ushindwe kulala naye. Huu ni mwendelezo wa kanuni za sekunde 7. Kama sekunde 7 hazikufanikiwa usijali, bado unazo nyingine 23 za kufanya maajabu.

Mambo 8 ya kufanya na kutokufanya ili kumvutia ndani ya sekunde 7


Je, bado unataka umshangaze ndai ya sekunde 7? Unajiuliza ni kwa ufanisi gani unaweza kuutumia huo muda? Mambo yafuatayo yatakusaidia kujua mambo ya kufanya au kutokufanya wakati upo naye kwa muda huo, au angalao kukuacha na tumaini kwamba amekuelewa.

#1 Usianze na misemo ya kawaida, mfano "Hivi uliumia ulivyodondoka kutoka mbinguni?..." Haya ni mambo ya kizamani, na hayatumiki katika huu ulimwengu wa kidijitali. Pia unatakiwa sana kuepuka kutoa tamko lolote kuhusu mwili wake mfano makalio, nywele, kifua, au kumuuliza maswali ambayo ni kuntu(personal) - mfano *Hello, kifua chako kinavutia*... Kiukweli, hayo mambo yatamfanya akuchukie chini ya sekunde tano, na hautakuwa na cha kumvutia mana umeshindwa kudhihirisha utofauti wako na wanaume wengine. 

#2 Sema kitu cha kufurahisha kidogo. Moja ya kitu kikubwa cha kumshangaza mwanamke ni kumtikisha mshipa wake wa kicheko / tabasamu. Hii inamaanish - kitu kikubwa unachotakiwa ukifanye ndani ya sekunde 7 ni kumfanya acheke.Mwisho wa siku hatakumbuka rangi yako ilikuwa ya aina gai, au ulivaa nguo gani - na badala yake atakuwa anakumbuka kitu kilichomfanya acheke.

#3 Usitoke nje ya mada. Usije ukaanza kumuelezea matatizo yako - kwamba jana ulipigana na X ukatenguka mguu, au kaka yako anamatatizo na mpenzi wake, au mama yako hupigwa na baba yako kila siku, au jinsi mpenzi wako wa zamani alivyo kuumiza moyo. Hii siyo target yako ya kutumia sekunde 7 kiufanisi, si ndiyo?. Achana na ya pembeni, ongea u fanya jambo litakalowagusa nyie wawili.

#4 Tumia misemo. Wanawake hupenda misemo; kwanza inakufanya uonekane msomi, mwerevu wa akili(intellecual), mwenye - mvuto, na wa ajabu - mysterious. Jitahidi kutafuta misemo na uiweke kichwani - uweke uhalisia wakati unaitamka - vinginevyo utakuwa kituko flani amaizing.

#5 Usiongelee ukubwa wa maumbile yako ya mwili. Ever. Kama anataka kujua, atagundua mwenyewe ila usiongelee kabisa hayo maswala.

#6 Muulize maswali yatakayomfanya aongee. Kama unaweza kumuuliza maswali yatakayomfaya afunguke na asiwe na doubt kuhusu wewe ujue hapo ushajichukulia point. Haijalishi wewe ni nani, ila kila mtu hupenda sana kuongelea maswala yanayomuhusu tena pale yaapokua ya msingi.
Muulize maswali kama:- Alizaliwa wapi - kalelewa wapi, Anapenda kufanya nini katika maisha - anataka kuwa nani, ni likizo gani ilimfurahisha kuliko zote, na muda siyo mrefu utakuta maongezi yanaenda hata zaidi ya dakika. Mojawapo ya vitu vinavyoweza kumvutia ni kumuonesha kuwa anaweza kuwa huru kwako - na ajisikie salama(confortable), kwa hivyo utaweza kumteka na akaongea vingi. 

#7 Usimshikeshike. Kusalimiana na kupeana mikono ni njia inayokubalika popote - inaonesha unaheshima kwake pale mnapotaka kuanza maongezi, lakini ikiwa baada ya kujitamblisha - utajikuta unamshikashika au kumtomasa - utajishushia heshima na utamchukiza mana itakuwa ishara ya dharau na hivyo utamkosa. Kuwa mwangalifu na mikono yako mzee - siyo kila msichana ni rahisi kiivyo!..

#8 Kuwa mwema. Amini usiamini - siyo mara nyingi watu huupokea ukarimu wakati wanapokutana na watu wasiowajua *strangers*. Mfano, Tuseme umemwona msichana mzuri kwenye mgahawa au sehemu. Kama kweli amekuvutia - badala ya kumwambia "nimekupenda toka ukiwa mbali", kwanini usimuagizie kahawa badala ya kupanga foleni, au ukamfungulia mlango wakati anaondoka, au kumpa tu tabasamu zito. Vitu hivyo vitamfanya akuone ni rafiki na kukupa nafasi ya kuongea naye pale unapohitaji.

No comments:

Powered by Blogger.