Mambo 10 Kutoka kwake yanayoashiria kuwa mpenzi wako ni husband material
Husband Material na Boyfriend Material ni watu wawili tofauti. Tambua kama mpenzi wako ni Mume au mwanaume kupitia tips hizi
Kama upo katika uhusiano, na ukaanza kuwaza kuhusu maisha yenu ya baadae, unaweza kuwa unajiuliza je "huyu ndiye sahihi?" au unajichimbia shimo lako mwenyewe ambalo hutaweza kutoka. Sasa mwanaume unayetoka naye anaweza kuwa mwanaume mzuri wa kutoka naye lakini siyo mwanaume anayeweza kukumudu katika maisha yako na kuishi naye kama mume wako.Na bahati mbaya hakuna kitu
au mtu anayeweza kukufata moja kwa moja kukuambia hili jambo moja kwa moja. Mara nyingi watu hutazama mitazamo yao inapokuja kwenye jambo linalouhusu moyo wako - hata marafiki zako unaweza usiwasikilize. Lakini tatizo ni kwamba hata mambo yako ya ndani yanahitaji ushauri wakati mwingine.
Utajuaje kama ni Husband Material?
Je umeshindwa kuelewa mawazo yako yanakuambia nini kuhusu yeye kuwa anafaa au la? Hizi ni mbinu rahisi unazoweza kuzitumia naukagundua kama mwanaume wako ni husband material.
#1 Anakufanya ujisikie na ujione mzuri ndani na nje, Hata iweje. Kama mwanaume wako anakusifia na kukwambia wewe ni mzuri hatakama kwa muda huo unahisi hauvutii, huyo ni fundi. Kama anakufanya utabasamu muda wote, kwa sababu anajua wewe ni mzuri na mwema, bado yeye ni fundi - anafaa. Kama utakuwa na mtu ambaye anakufanya usijiamini, hali itakuwa mbaya zaidi pale unapo anza kuzeeka / kuwa mama. Kama mwanaume kweli anakupenda atakupenda kwa kila kitu ulichonacho.
Hakuna dhaifu ylako lolote litakalomfanya atoke kwako - hata syiku moja. Wote kwa sasa mnaweza mkaonekana wazuri lakini kadri umri unavyozidi kwenda, mambo yanabadilika. Kumbuka , unahitaji kuwa na mtu atakayekupenda wewe ulivyo nje na ndani, kwa mazuri yako na mabaya yako.
#2 Ni mshabiki wako mkubwa sana(Ni supporter wako mkubwa). Kama unatoka na mwanaume ambaye anaku sapoti kwa mambo mengi, hapo ujue upo na mtu sahihi. Kama unafikia hatua ya kujaribu kitu kipya, au una mpango wa kuanza biashara mpya siku zote anakuwa makini kukusikiliza na kulisapoti wazo lako. Unapokuwa katika uhusiano unahitaji kuwa na mtu ambaye atyakufanya ujisikie furahana kukuheshimu wewe pamoja na mawazo yako.
Unapokuwa na mwanaume ambaye anakufanya usiwe na amani na kukuona wewe mjinga kwa mambo yako unayofanya au unayopanga kuyafanya. Maisha yanakuwa mafupi na magumu sana unapokuwa na mtu ambaye anakuzuzua akili yako na kuonesha kutokuwa na imani na wewe.
#3 Muda wote anatamani awe na wewe. Kama upo na mwanaume ambaye anapenda kukushika, kukubusu, kuku-kumbatia, na mengine kama hayo, ujue huyo anafaa. Kama upo na mwanaume kwa mwaka mmoja, au miwili au zaidi ambaye anakukiss na kukupenda kama vile mmekutana jana ujue upo na mwanaume sahihi. Unahitaji kuwa na mtu ambaye muda wote anakuhitaji, mtu ambaye anakupenda kila kukicha - hakuchoki, ambaye upendo wake wa sasa ni sawa na wa mwaka jana/ juzi.
Kama mwanaume wako upendo wake umeshuka na unazidi kushuka kadri siku zinavyozidi kwenda na wewe ukagundua hilo, ujue huyo siyo mwanaume wa kuolewa naye. Unahitaji kuwa na mtu anayekuhitaji kwa muda wote, na wakati wote.
#4 Anakuongelea na anajisifia kwa rafiki zake kwa kuwa na wewe. Kama upo na mwanaume ambaye haogopi wala hasiti kupost picha mlizopiga wawili katika mitandao yake ya kijamii, au anawaambia marafiki zake jinsi ulivyofaulu mtihani mkubwa aliokupa, au kama anakusifu kwa jinsi alivyokuona wa tofauti, ujue huyo ni material. Kama mwanaume uliye nae anakusifia kwa rafiki zake na kwa familia yake kwa jinsi wewe ilivyo wa tofauti ujue huyo anafaa kuwa baba watoto wako.
Kumbuka, unahitaji kuwa na mwanaume ambaye anakutazama na kukuongelea kwa mtazamo chanya, mwanaume ambaye anajisifu kuwa na wewe, na anajiona wa heshima kuwa na wewe. Kama mwanaume anakupenda, hatasita kuwaambia wengine jinsi wewe ulivyo mwema na mambo mazuri unayomfanyia, na lazima akusifie mana anakupenda sana.
#5 Amehamasika. Amehamasika na kutiwa moyo wa kufanya kazi kwa bidii, na anataka afanikiwe katika maisha kwa sababu anatarajia kuwa na familia na watoto, na aweze kuihi na wewe maisha marefu ya furaha pamoja na wewe. Hupendi kuishii na mwanaume ambaye ni keeper, ambaye ana miaka 34 lakini bado anaishi kwa wazazi wake na kula vya wazazi wake, au mwanaume ambaye ni mtoto wa mama ambaye hata wakati mwingine ukiwa naye unaogopa atakuaibisha / hatakulinda.
Unahitaji kuwa na mwanaume ambaye anajitegemea na anaweza kuendesha mambo yake bila utegemezi, ambaye anapenda kujifunza jinsi ya kupika, na ambaye ni mzuri ambaye ni mzuri katika kutatua changamoto ndogondogo zilizopo nyumbani. Kama una date na mwanaume ambaye ana maadili katika kazi, mwanaume ambaye kajiwekea malengo yake, tambua huyo ni hubby material.
#6 Familia ni kitu cha muhimu kwake. Unapokuwa unawaza kuishi na mwanaume katika maisha yako, ni muhimu kuhusisha na kutambua ni mambo gani mnayaona ya msingi, na ya pamoja. Kama familia ni muhimu sana kwake, na yupo karibu sana na familia yake(wazazi na ndugu zake), uwezekano wa kuwa baba mzuri baadye ni mkubwa.
Unahitaji mwanaume ambaye anaithamini familia, na ambaye anaelewa ina maana gani kubwa ya kula chakula cha pamoja jioni na watoto na sio tu ilimradi chakula cha jioni. Kama anaithamini familia yake, basi anaiheshimu, na heshima ni kila kitu tena hasa kwa mwanaume ambaye unataka uwe nae maishani. Kama umeishi na mwanaume zaidi ya mwaka, na haujawahi hata siku moja kumuona akiwa na macho ya wasiwasi, basi huyo usimwache. Mwanaume anapokuwa anakupenda, anakuwa kama kitabu kilicho wazi, na atakiweka kitabu chake wazi siku zote. Na wewe pia utakifungua cha kwako!. Hajali wala haogopi ukichukua smart phone yake kama unataka kuiangalia au kuitumia. Hawezi kukukasirikia wala kukufokea kwa wewe kuichukua laptop yake na kuangalia emails zake. Pia hajali kama utakuwa kama crazy girl ambaye anapenda kuwa na staffs zake nyingi kwa wakati mwingi.
Wewe ni mtu wake wa pekee, na analijua hilo - hivyo hana haja ya kuogopa. Siku zote anajiamini hata ufanye suprise gani. Na wewe hiki ndicho unachokipenda kwake, na unajua kabisa ya kuwa hawezi kukuumiza, kwa sababu unajua kweli anakupenda. Kama kweli una mwanaume wa hivi, Hiyo ni keki shoga Usiiache - Mjali kwa vyote!.
#8 Anayafanya maisha yako kuwa marahisi unaokuwa nae. Kama kweli unampenda mpenzi wako, hauwezi kumchoka. Unaweza jikuta upo mwenyewe nyumbani umelala kwenye kochi na yeye yuko mbali, na ukaanza kuwaza angekuwa nyumbani angekuwa mbele yako anakuchezea kama Mr.Bean au mfanya matangazo ya biashara. Au labda utaimisi sauti yake akiwa sebuleni kila siku jioni akiwa anaangalia mpira kwenye TV.
Kama kweli hatakama hayupo nyumbani na wewe upo peke yako home na kumkumbuka tu kunakufanya utabasamu, huyo usimuache. Kama kweli umefikia hatua ya wewe kujiuliza kabla yake ulikua unaishije bila yeye huyo usimuache. Unapenda kuolewa na mwanaume ambaye atakufanya utabasamu muda wote na si yeye akiwepo tu, mwanaume ambaye anapenda unuse harufu ya maua ya Upendo muda wote!.
#9 Ni mvumilivu. Hii ni muhimu sana, kwa sababu "Uvumilivu ni Tunu na ni kipawa", na "mambo mazuri huja kwa wale wanaosubiri." Na wewe umekuwa mpole muda wote huo ukimsubiri mwanaume mtulivu ambaye utaolewa nae, na sasa unajihisi na unaona unaye / umempata. Unapofikiriwa kuhusu kuolewa na mwanaume, unatakiwa ujue utu wake anapokuwa amekasirika, au kachanganywa na mambo(Frustrated), na ufikirie na kujiuliza anakuwa na muitikio gani hasa pale wewe unapokuwa umemkasirisha.
#10 Mcha Mungu. Mwisho wa yote ni hili, maana kama mwanaume ni mcha Mungu hawezi kufanya jambo lolote la kipuuzi maana ni kinyume na maandiko matakatifu kwenye Quran na Kwene Biblia. Hii itakuza maisha yenu ya kiroho na mtakuwa na familia ya amani mana wote mnayo hofu ya Mungu ndani yenu
Kila mwanamke anaweza kuwa na mtazamo wake binafsi wa mtu anayeitwa "husband material", lakini haya mambo 10 yanatengeneza msingi wa mengine yote, na ndiyo yatakayokufanya ujue yeye "Ndiye"!.
Kama imekufungua na imekusaidia kujibu maswali mengi uliyokuwa ukijiuliza basi share na shosti wako ili imsaidie kama ilivyokusaidia wewe.
No comments: