Sababu 11 za kwanini hajakuomba muoane!
Je umekuwa na boyfriend wako kwa muda mmrefu na unaanza kujiuliza kamakweli atakuomba muoane au la? Tutakusaidia kujua kikwazo ni nini - nini kinamshika!..
Kwa wanawake wengi, kuolewa ni mojawapo yao makubwa katika maisha. Huwa wanawaza pete za dhahabu vidoleni mwao, magauni ya harusi, na anawaza kuyasema yale maneno "ndiyo nakubali kuwa wako milele" mbele ya rafiki zake wote na umati mkubwa. Vilevile, wanaume wengi wazo la ndoa haliteki akili zao kama wanawake. Japo, wazo la kuoa ni la muhimu pia kwao, lakini hawaendeshwi na wazo zima la kumvisha mwanamke pete, na kwenda kujitambulisha kwa wazazi wa mwanamke na ishu nzima ya ndoa!.
Kwanini bado hajakuomba muoane?
Kama unajiuliza kwanini hajaanza kuku-uliza maswali yanayoelekea huko, yafuatayo ni baadhi ya mawazo yanayoweza kuwa yanazunguka katika akili yake!..
#1 Ni mwangalifu sana kwenye Viapo / ahadi zake. Baadhi ya wanaume wanaogopa sana kula viapo mana wanaogopa jambo hilo linaweza kuwa pigo kwao. Inaweza ikawa ni kwasababu alishakuwa na historia mbaya kuhusiana na mapenzi, labda mpenzi wake alimfanyia mambo ambayo siyo na akamgeuka, au vitisho vingine vinavyohusiana na hivyo vinaweza kuwa vimemtisha.
Haya mambo ya kujiwekea nadhiri yanaweza kusuluhika/ kushughulikiwa. Japo, itamgarimu muda sana kwa hilo wazo la kuoana kumuingia akilini, hivyo atakuwa anahitaji muda wa kulifikiria hilo swala kwa kina.
#2 Anawasiwasi kwamba ataukosa uhuru wake aliouzoea. Kwake, kuoana inaweza kuashiria kuongezeka kwa majukumu, tena hasa pale mnapoanza kuwa na watoto. Boyfriend wako anaweza akawa anajiuliza kuwa - ni vitu gani atavikosa akishakuweka ndani, na kutokana na hivyo vitu ni bora abaki bachelor au akuoe?
#3 Labda yupo bize sana kwa sasa. Kunamuda, maisha yanakuwa yamekukaba na unakuwa bize sana na kazi nyingi kujikwamua kiuchumi. Na kupanga kuhusu mambo ya ndao itagarimu muda na nguvu nyingi. Labda ndo mana boyfriend wako hawezi kuliweka kwenye ratiba yake kwa sasa. Kama anapitia katika kipindi cha muhimu sana katika kazi yake, au familia yake, wazo la ndoa / kuoana linaweza kuwa la mwisho kabisa katika ubongo wake. Lakini hakuna anayejua kitakachotokea miezi michache ijayo - mambo yanaweza kuwa mazuri na kubadilika na ukaolewa mwaka huohuo.Kinachotakiwa ni wewe kumsoma mwenzio anapitia katika kipindi gani.
#4 Labda bado anampenda sana mpenzi wake wa zamani. Mara nyingi, hii haitokei sana, lakini kama boyfriend wako hakuombi muoane, inawezekana bado anamkumbuka mpenzi wake wa zamani. Kama bado ana Like picha zake na luandika comments nzuri katika picha zake za Instagram, au kuongea na e mara nyingi, hizo zinaweza kuwa ishara za hatari.
#5 Anauhusiano mwingine na msichana mwingine mbali na X wake. Kama umegundua kuwa mwanaume wako anatabia ya kutoka out na mwanamke mwingine mzuri eti kwa kisingizio ni rafiki yake sana, au labda ni mfanyakazi mwenzake, au mwalimu wake wa mazoezi, au walisoma wote, inatakiwa umwe mwangalifu sana mana utakuwa unaibiwa. Mara nyingi wanaume wengi hawaupeleki uhusiano wenu level nyingine kama kuna upande mwingine unamvuta.
#6 Hajanunua pete bado. Hili ni jambo la kawaida linalojulikana kwamba wanaume wengi hawana hobby ya kufanya shopping kama wanawake walivyo - Hii ni tabia asilia. Pete ya uchumba / ndoa ni kitu cha muhimu sana kununua, na mwanaume wako kanyamaza, kwa sababu anaweza kuwa anaogopa kuwa hatapata ile anayoitaka au unayoitaka.
Kama hii ndo sababu, basi anaweza kuwa anawaza kuhusu ndoa muda si mrefu ujao. Sasa kinachotakiwa ni msaada kidogo wa kumsaidia ainunue hiyo pete.
#7 Inawezekana kanyamaza kwa sababu anataka amuombe baba yako kwanza ruhusa. Licha ya ukweli kwamba nyakati zimebadilika, wapenzi wengi bado hupenda ule mfumo wa kitamaduni inapokuja katika ishu ya uchumba na ndoa. Moja wapo ya mambo yaliyozoeleka katika hizi tamaduni ni kwa mwanaume kumuomba baba wa mwanamke ruhusa ya kumchumbia na kumuoa binti yake.
Sasa kama boyfriend wako ana uhusiano mdogo sana na baba yako - hajazoeana sana na baba yako, hiki kinaweza kuwa kikwazo cha yeye kuomba kukuchumbia/kukuoa. Boyfriend wako anaweza kuwa na mawazo kwamba, Baba yako anaweza akakataa. Na hii inamuiwa vigumu sana yeye, kwa sababu anakupenda sana na anataka akuoe. Na inawezekana anatafuta mbinu bora sana ya yeye kumuingia baba yako ili asiweze kumkatalia.
#8 Inawezekana anasubiri kwanza kaka yake mkubwa amuoe kwanza mpenzi wake. Mara nyingi, Kaka kama inavyofanana kwa kwa dada, wana mstari fulani kwenye ishu ya kuoa/kuolewa. Kaka mkubwa lazima ategemee kwamba mdogo wake atamsubiri kwanza yeye aoe kwanza ndipo mdogo afuate. Na kwamba mdogo mtu asipoufata huo utaratibu inaonekana ni ukosefu wa heshima. Kwa hiyo kama mpenzi wako ana kaka yake ambaye hajaoa - hii ndiyo inaweza kuwa sababu dear!.
#9 Inawezekana anaogopa kuwa baba. Hii inawezakuwa sababu kubwa inayomfanya asikuombe muoane kwa sababu, wanaume wengi hawanaga uhakika kama kweli wapo tayari kuwa baba, au wana wasiwasi - nitaweza kufanya kazi zangu sawasawa na kutimiza wajibu wangu wa kuwa baba bora kwa pamoja?, hatakama tayari inaonekana anajimudu.
Kuwa baba inamaanisha kuwa na uwezo wa kumudu mahitaji yote ya kwako, mkeo, na kuweza kuwakuza watoto mpaka watakapokuwa watu wazima. Ni kazi kubwa sana, na boyfriend wako anaweza kuwa anakosa kujiamini kama anaweza timiza huu wajibu mzito. Hivyo, inatakiwa ujadiliane naye kama kuna kitu ana wasiwasi nacho.
#10 Hataki kuwa mwanaume pekee aliyeoa katika kundi la marafiki zake. Kama mpenzi wako ana marafiki wengi ambao bado hawajaoa, hii inaweza kuwa sababu ya yeye kuchelewa kukuomba muoane. Kwa yeye kuwa wa kwanza kuingia katika ndoa inaweza kuwa ngumu kwa sababu anahitaji asikilizie kwa wenzake ndoa iko vipi, ni nzuri au ngumu.
Kama utagundua kuwa marafiki zake wengi bado hawajaoa, au wapo katika mahusiano lakini bado kuoana, Hiki ndicho kikwazo Shosti. Sasa: Kama kuna njia yeyote kuna njia yeyote ambayo unaweza kuitumia kuwafanya marafiki zake waweze kuitamani ndoa - basi itumie hiyo njia itasaidia. Kwa sababu wanaume wengi hutegemea ushauri wa wenzao katika maamuzi magumu kama ya ndoa.
#11 Inawezekana kuna mambo mengi ambayo bado anahitaji kuyakamilisha kwanza kwenye maisha yake. Ndoa ni mwisho wa yeye kuwa na maisha ya kuwa single na free. Inawezekana mpenzi wako bado hajaenda katika ile Safari yake ya Ulaya, au bado hajanunua ile kampuni bado.
Kabla hajaanza kuwaza namna ya kuijenga familia, inawezekana anataka kufanya kitu kikubwa kwanza. Na hivyo anahisi, akishakuwa na mke na watoto hataweza tena kutimiza malengo yake. Ila usijali, hapa ndipo unatakiwa mwanamke wa nguvu kuhakikisha anafikia ndoto zake haraka iwezekanavyo.
No comments: