Mambo 15 unayoyahitaji kuwa mwanaume wa kweli
Mwanaume halisi hapimwi tu kwa maneno yake, au muonekano. Ni mtu ambaye siku zote hutazamiwa na hupewa heshima katika jamii inayomzunguka. Na ndiyo, ni mwanaume ambaye anajua ni jinsi gani ya kuishi na wanawake pia.
Kuna wanaume wengi sana ambao wao hupenda au hutamani wapendwe au waonekane wema, wengine hupenda wavutie.
Unachotakiwa kufanya ni kuwa wewe, kuza ufahamu wako na sura zote za maisha yako
Mwanaume halisi hana ngozi nene kuliko wenzake. Uanaume halisi utengenezwa ndani ya mtu, na udhihirika tu kwa
nje.
Ikiwa kweli unataka kuwa mwanaume halisi na kujijengea heshima katika jamii, haya mambo 15 yatakusaidia sana kama utayaingiza katika maisha yako ya kila siku.
Siyo kitu ambacho kinaweza kubadilishwa ndani ya siku ,moja au mbili, lakini kitu ambacho unatakiwa kufanya ni kuvitekeleza taratibu katika maisha yako ya kila siku, ukiwa na nia hiyo muda si mwingi utakuwa mwanaume uliyekuwa ukitamanai kuwa.
Kuwa na Kanuni na taratibu zako(Have your Principles). Hizi ndizo zinazokutambulisha wewe na kukufanya wewe kuwa wewe. Je wewe una kanuni zinazokuongoza katika shughuli zako za kimaisha za kila siku?. Mwanaume mwenye kanuni ni mwanaume anayeilinda imani yake, anayetambua hili ni zuri na hili ni baya. Kanuni zinamfanya mtu awe wa viwango vingine kitabia mana hatakama unapenda kufana kitu fulani lakini kikakinzana na kanuni zako, hautakifanya, hivyo zinakusaidia wewe kutofautisha hisia na uhalisia.
Unaweza kumuua mtu kwa sababu ya fedha? Au unaweza kufana mapenzi na mwanamke kwa sababu tu alikua amelewa na hajitambui?. Nadhani angalao utakua umepata picha.Mwanaume mwenye kanuni ni mtu ambaye anaweza kushabiiana na tukio katika wakati wowote anapokumbana na jambo. Haimaanishi kwamba mtu huyo hawezi kubadilika kutokana na kauni zake, hasha, ila anaweza kubadilika kutokana na muda(wakati).Hivyo kanuni zinamsaidia mtu kutofautisha kitu kizuri na kibaya.
#2 Sheria hizohizo zinafatwa na kwa mwingine. Watu wengi sana duniani hawazingatii hili jambo. Mwanaume hufata sheria kuu(Universal Rules) ambazo atazitumia kwa yeye binafsi na kwa wengine. Kama utategemea mtu akutake radhi kwa sababu kachelewa kufika , nawe pia uwe na radhi pale unapochelewa pia. Kama hautaki mwanamke wako awe anawangalia wanaume, nawe pia usiwe unawatolea macho wanawake wengine. Mwanaume halisi hana wivu(upendeleo), pia haweki sheria za kwake zikatofautiana na za wengine.
#3 Neno lake ni neno lake. Wakati mwanaume anapoweka ahadi, ataisimamia mpaka aitimize hata iweje. Watu wengi wanaweza wasielewe hili jambo, lakini hakuna kitu kinacho mpa mwanaume heshima kama pale anapoisimamia ahadi aliyoiweka kwa mwanamke wake bila kuyumbishwa mpaka aitimize.
#4 Mwanaume wa kweli ni mwenye busara. Mwanaume wa kweli huwa na heshima na ukarimu. Mwanaume wa kweli hujua jinsi ya kuenenda akiwa na mwanamke. Anamjali mwanamke wake au mchumba wake kwa upendo na hisia, na siku zote anakua anatenda mambo huku akimuheshimu mpenziwe. Siku zote ni nguzo ya mwanamke wake na hutimiza mahitaji na matamanio ya mpenziwe.
#5 Heshima na Ubinadamu. Mwanaume wa kweli siku zote ni mpole na huwapenda wanaomzunguka bila kujali tofauti zao. Siyo hiyo tu, huwa ana harufu ya mamlaka(authority) pamoja na kujiamini na mwenye kutoa maamuzi yakinifu. Huwaheshimu na kuwapenda wanawake wa aina yeyote bila ya kujali umri wao,na hawezi kuwakosea heshima au kuwadhalilisha.
#6 Mwanaume wa kweli ana ndoto. Anafata ndoto zake kwa jitihada zote na kwa furaha bila majuto wala kusita. Mwanaume wa kweli huyaweka maisha yake rehani kwa ajili ya ndoto zake,lakini wakati huo huo haimfanyi yeye kusahau au kuacha kutimiza ahadi alizoziweka kwa mwanamke anayempenda. Haijalishi atakua bize kiasi gani, bado hutenga muda wake mdogo kwa ajili ya yule anayempenda.
#7 Mtanashati na maridadi. Mwanaume wa kweli hababaishwi na vipodozi, lakini hujua jinsi ya kujitunza na kujiweka msafi wakati wote. Muda wote huvaa vizuri na huwa mwangalifu sana kuchagua mavazi yake ili muonekano wake usije ukaharibiwa. Kwa hiyo kama unapenda kuwa mwanaume wa kweli kuwa mtanashati hakuna mwanamke anayeweza kukupinga.
#8 Anauelewa wa kila kitu kinachomzunguka. Mwanaume wa kweli hakosi ufahamu. Huwa na uelewa wa mambo yanayomzunguka na uhakikisha anapata habari zote za masuala yanayo muhusu iwe mazingira, watu na hata siasa za nchi na kimataifa. Ni mwerevu wa akili(Intelligent), mtu wa watu na mwenye kuaminika kwa kutoa ushauri mzuri wakati anapo ombwa kutoa.
#9 Ni mtu wa staha(mannered). Anakua mpole anapotakiwa, na anatoa msaada pale anapoona mtu anauhitaji. Hatoi chochote kwa mtu yeyote, mana hawezi kuwasaidia watu ambao hawaitaji msaada, kwa maneno mengine, hamsaidii mtu bila sababu. Mwanaume wa kweli huwasaidia wahitaji.
#10 Anajitabua(Determined). Ana upendo na ni mwaminifu kwa ndoto zake na maono yake. Hayakimbii matatizo wala changamoto bali huzitatua. Hupanga malengo yake na kuweka njia nzuri ya kuyafikia kwa kujiamini na kujielewa.[Soma: Jinsi ya kufanikiwa kimaisha].
#11 Hajifichi, hutembea kwa kujiamini. Harudi nyuma wala kujificha kama mwizi au kibaka. Hupenda uwepo wake mahali utambulike kwa heshma zote. Anajiheshimu hivyo haoni haja ya yeye kuonekana dhaifu mbele ya wengine.
#12 Mwanaume wa kweli sio Mnafiki. Ni mwaminifu katika mawasiliano na matendo yake. Hayumbishi maneno Cheupe hukiita Cheupe na si vinginevyo, huwa mkweli pale ukweli unapohitajika hapepesi macho, labda tu pale anapoona kuna haja ya kuficha ukweli ili kuepusha kitu kibaya kutokea.Lakini, sio rahisi kuyumbishwa na haogopi kuchukiwa kwa sababu ya kusema ukweli.
#13 Anayamudu mambo yake(He is in Control). Anayamudu na kuyaendesha vizuri maisha yake. Mkimya na bado mwenye kujiamini hata pale mambo yanapomuendea kombo, hakati tamaa. Mwanaume wa kweli hujua kupanic na misongo ya mawazo itamfanya yeye asiwe fanisi katika mambo yake na kutamletea woga. Hupanga, na kufanya maamuzi na kusubiri matokeo ya kazi zake katika hali ya utulivu wa nafsi na akili.
#14 Hutambua na kuziona Fursa zinazomzunguka. Je, unajua kitu kinachokufaa sana?, na Je, unajua kitu ambacho unaweza kukifanya kikakufanya mkamilifu katika maisha?. Wanaume wengi sana huchanganyikiwa sana katika kutambua fursa zinazoshabiiana nao. Tambua Fursa itakayokupendeza wewe na itakayokufanya wewe ukose usingizi, unayoipenda.
#15 Mwanaume wa kweli huyakubali makosa yake. Kubali makosa yako pale inapotokea, na usiyarudie tena wakati mwingine. Mwanaume wa kweli hatupi lawama kwa wengine kama ilikua makosa yake kwa jambo fulani kutokea. Huyakubali makosa yake na kuhakikisha hayajitokezi tena. Anaelewa kwamba, kukubali makosa hakumfanyi yeye kuonekana kuwa kashindwa au dhaifu. Inamfanya yeye kuwa shujaa na mwenye kujiamini zaidi.
Ni jisi gani ya kuwa na mwonekano wa Mwanaume wa kweli na kutenda kama mwanaume wa kweli?
#1 Usiogope wala usicheke kwa uoga(dont giggle). Kama jambo limekuchekesha Furahi, tena cheka kwa nguvu. Kama hakichekeshi, tulia.
#2 Kuwa na Mustache. Kama hiyo haidhidirishi wewe ni mwanaume. Kipi kingine?
#3 Kama wewe ni mnywaji, kuwa na whiskey nyumbani kwako. Hatakama umepanga. Jifurahishe mwenyewe kwanza kabla mwingine hajaja kukufarisha.
#4 Usiogope kumwangalia mtu(Eye Contact). Hautakiwi kuwa mtu wa kupepesa macho. Kunakufanya wewe uonekane mwanaume wa kweli tena unayejiamini.
#5 Usijiingize kwenye maongezi ya kitoto. Kuwa mkimya kama mada ni ya kipuuzi.
No comments: