Tofauti Kati Ya Urafiki Wa Kawaida Na Urafiki Wa Kimapenzi
Kwa miaka miwili sasa nimekuwa nikifundisha mahusiano kwa kulenga Nature ya Binadamu. Pia natamani kuingia ndani zaidi ili kuboresha mahusiano ya kila aina.
Kitu ambacho nimekipata wanafunzi wangu mfurahie kujifunza zaidi kuhusiana na haya mahusiano, Ni ufunguo wa kila sekta inayoleta urafiki wa kimapenzi
Nature ya mahusiano ya kawaida inatofautiana na mahusiano ya kimapenzi kwa njia hizi , Ufahamu, kutegemeana , kujali, tumaini, mwitikio, kujitolea na Uongozi.
1.Ufahamu
Tunapotaka kutengeneza mahusiano ya kimapenzi tunapenda kufahamu kwa undani zaidi , ili mtu ajisikie vizuri na awe wazi kwa mwenzake. Kiasi cha taarifa ambazo tunapeana ni za kutosha kutoka kwa mtu mmoja na mwingine. Huwa tunajitahidi kutafuta taarifa kwa marafiki wa karibu na hata ndugu na watu ambao tayari ni wenza.
Hasa kwa upande wa wanaume kuna vitu vingi vya kufahamu ili kupata wenza wa kimapenzi katika mahusiano mazuri, hujisikia salama wanaposikia kuwa na ndoto kubwa ya ndani , matamanio, hofu, mambo yaliopita, malengo kwa ajili ya baadae.
2.Kutegemeana.
Watu ambao wapo kwenye mahusiano ya kimapenzi mara nyingi hutegemeana , kila mwenza humtegemea mwenzake, wakimaanisha, mara kwa mara katika kuweka umuhimu wa kila mtu. Hii inaweza kuingia katika kuchagua kitu gani cha kula , mahali gani pa kuishi.
3.Kujali, kuhudumiana, kutunzana
Kumjali mwenza ni aina ya urafiki wa mahusiano ya kudumu ya kimapenzi. Na hapa kinachotofautisha ni kila mtu kukaa mahali pake na hakuna kumjali mwingine kwa lolote. Kuishi pamoja ni hali ya ustawi kwa wanadamu yeyote ambaye ana mahusiano mazuri. Vinginevyo mtu anaweza kuishi kwa stress, bila usalama japo ni aina ya mawasiliano, au jinsi gani utaonyesha upendo. kwa mfano wenza hutamani kuonyeshwa uaminifu, kujaliana kwa kila mtu.
4.Tumaini.
Kwa maoni yangu mwenyewe, tumaini ndilo huweka mapenzi vizuri, Wakati inapokuwa ngumu kuwa na tumaini mtu hawezi kujisikia vizuri , hana ustawi . Kwa maana nyingine ni kwamba ni ujasiri unaomletea kila mtu kuwa na heshima, haki, na kupata faida . Bila ya kukutana na madhara yeyote
5.Mwitikio.
Mahusiano mazuri hutokana na mwitikio au kujitoa kwa mtu. Na kila upande uwe umejitoa kwa mwenzake katika kila hitaji . Ina maana ya kutambua, kuelewa na kusaidiana kila mmoja katika nyakati zote nzuri na mbaya. Kupoteza kazi, kupata ujauzito, kupandishwa cheo, . Kama kila mwenza atakutana na hitaji la mwenzake, itaonyesha makubaliano , kukubalika kila upande. Kila mtu atajisikia kupendwa.
6.Uongizi
Kukiwa na mahusiano mazuri kila mwenza atakuwa anatambua na kufahamu kuwa sio yeye bali ni wao kwa kila kitu , mtazamo huu ni mzuri . kukiwa na mahusiano ya ndani kabisa wenza wote lazima kubadilisha mtazamo wao. kujua kabisa kila kitu wanashare, sio mbili bali ni moja.
7.Kujitolea au sharti
Mwisho katika mahusiano mazuri, kuna kujitolea ili kuendeleza uzuri wa mapenzi ili kila mtu afurahie sehemu yake na akue vizuri kiakili, kiroho na kimwili. Kwa kuwa na wazo kwamba mahusiano yanatakiwa kupaliliwa , kumwagiliwa maji , kuwekewa mbolea na kila siku kuangalia mahali popote kama kuna adui kaweka magugu ili uweze kuondoa mapema kabla ya kuharibu mmea.
Uongozi unahusu wenza wote . kuonyesha kujali, kuweka nguvu kwenye kujitolea na kuwa na mwitikio pande zote.
No comments: