Siri Za Kudumisha Mahusiano Yako

Jinsi ya kuyafanya mahusiano yako yadumu.
Asilimia kubwa ya watu wanaouliza  kuwa, wanawezaje kudumisha mahusiano yao?
Zifuatazo ni mbinu 3.
1.Mwanaume asiruke Maandiko ya Imani yake.
Mwanaume anapofikia umri wa kuoa ni lazima kwanza amuombe Mungu kazi. Kwa sababu kazi yake ndio itachagua mwanamke wa kuishi naye ili ndoa au mahusiano yao yaweze kudumu.  Usiombe mkeMwanaume Omba kazi kwa Mungu. Mahusiano yanayodumu hayaletwi na mihemko ya mwili. Yanaletwa na ukomavu wa akili ya mtu , yanaletwa na  Upendo wa kweli, Upendo ambao huanzia kwenye urafiki wa kweli.
Kazi ya kuajiriwa ni kibarua, kazi ya kujiajiri ndio kazi. kazi ya kutumia akili yako, kazi ya kumiliki muda wako, wewe uwe ndio raisi wa muda wako.  ukiwa  na shule utapata mke mwalimu. ukiwa na Hospitali utapata mke Daktari au nesi, Ukiwa  mtumishi utapata mke mtumishi. Kazi ndio inayochagua mke sio maombi ya kila siku ya kupata mke mwema.
2.Inahitaji Kukamilishana.
1images_file_photo_689928633 Siri Za Kudumisha Mahusiano Yako
Tabia nzuri kwenye mahusiano ni katika kukamilishana.  Kama unasikia kuboreka kwenye mahusiano yako ni kitu cha hatari sana. Chumba cha kulala sio cha kusoma novelsoma nje ya chumba cha kulala.  mawasiliano ni muhimu kwa watu wawili. Kupeana muda wa kutosha. Hakuna zawadi kubwa kama kumpa mwenza wako muda wa kutosha, kumsikiliza. kukutana na mahitaji ya kila mtu.
3.Kujitoa Kwa Bidii Kuboresha Mahusiano.
young-african-american-couple-remote-footage-000826510_prevstill-1-1024x576 Siri Za Kudumisha Mahusiano Yako
Wenza ni lazima kuamini kwamba mahusiano  yanajengwa na watu wawili sio mmoja . Kama mnataka mabadiliko , kila mtu aangalie upande wake . Abadilike yeye kwanza . hutaweza kumbadilisha mtu, Mungu peke yake ndio master wa kubadilisha watu.  Hakikisheni mnatafuta taarifa za kutosha kuhusu  kuendeleza mapenzi yenu.  Ukiwa na taarifa za kutosha utakuwa na ufahamu, ukiwa na ufahamu utapata Hekima.
Kumbuka kuwa mtengeneza mahusiano na mvunja mahusiano sio mtu wa pembeni ni wewe mwenyewe. Mkielewa hili hakuna kitakachozuia  mahusiano yenu kudumu. Ni ujumbe mfupi lakini ukizingatia utakupa faida kubwa.

No comments:

Powered by Blogger.