Hivi Ndivyo Ambavyo Utampoteza Msichana Ambaye Tayari Anaipenda Nafsi Yake
Utampoteza pale ambapo utafanya mambo ya kijinga, kwa kufikiria kuwa atakubaliana na kila unachokitaka. Kwa kufikiri atakubaliana na muda wako wa kijinga usio na thamani kwake.
Utampoteza kwa kutomwambia jinsi gani ana thamani kwako. Kwa kutoweka alama ya mahusiano . kwa kumfanya afikirie kama unamjali au unajaribu kufanya hivyo.
Utampoteza kwa dalili zako za mchanganyiko, kwa kumweka sehemu yako ya pili kwa kila unachokifanya. kwa kushindwa kufikia kiwango alichonacho kwa watu waliomzunguka.
Utampoteza kwa kutojibu ujumbe kwa wakati, na kutegemea kuwa atakubembeleza kwa kukuuliza kwa nini hukufanya hivyo. Utampoteza kwa kuahirisha mipango kila mara na kutegemea atakuja kwako usiku ili kulazimisha kupeleka mipango yenu mbele.
Utampoteza kwa kufikiri kuwa kila mara atakutafuta ili awe karibu yako. kwa kufikiri kuwa unaweza kusema chochote kwake ili aweze kukaa na wewe. Elewa kwamba hawezi kufanya kitu hicho.
Utampoteza kwa kumpa nusu ya moyo wako kwa kufikiri kwamba atatosheka. kwa kuchukua kwake zaidi kuliko unavyotoa wewe. Kwa sababu hujali muda wakati mwingine hataweza kukuelewa. Hutafanikiwa kuwa naye.
Utampoteza kama utamchukulia moyo wake laini kirahisi. kwa kutokutambua uzuri alionao anapokuandikia ujumbe asubuhi kutaka kujua hali yako, hata wakati ukiwa kazini. kwa kutothamini vitu vidogo anavyofanya kwa ajili yako mbali na wema wa moyo wake.
Utampoteza kwa sababu macho yako hayatulii na yeye, kila mara akipita msichana mwingine unapeleka macho mpaka mwisho , unaonekana huna msimamo
Utampoteza kwa kuwa unamwangusha katika mambo mengi. amekupa nafasi hujaitumia vizuri. umemkatisha tamaa hata hawezi kukuamini katika maisha yake.
Utampoteza kwa akili yako ya kufikiria kuwa anaweza kukubaliana na aina hio ya mahusiano. kwa kutopokea simu, kutojibu meseji. kwa kufikiri kuwa hajali mahusiano yalio ya kweli na ya kudumu. Kwa kufikiri kwamba atakupa kila unachohitaji.
Utampoteza kwa kumfanya awe na shaka kwa ajili yake,Kwa kuanza kujiuliza maswali yanayostahili.Ataanza kujilaumu mwenyewe. Lakini atakumbuka tu kuwa anastahili kitu kingine sio hicho. Atatambua kuwa hana sababu ya kupoteza muda wake kwa mtu ambaye anamfanya ajisikie kama mtu asiyevutia, au asiye na upendo ndani yake. Ataamua tu kuwa wewe humfai hata kidogo. Ataamua kuondoka na hatarudi nyuma.
No comments: