Utajuaje Kama Mwenza Wako Hakupendi

Tofauti kati ya kupenda na kuwepo katika upendo.
Mungu ameagiza Upendo kwa kila mtu. tena aliagiza kumpenda jirani yako kama nafsi yako. Mungu anataka ujipende kwanza wewe ndipo utatambua jinsi ya kumpenda mwingine. Linda moyo wako kuliko chochote ukilindacho hapa Duniani.

Kama unatafuta kupendwa , ina maana ndani yako kumekosekana upendo.  Usipojaza hio nafsi , hutajua thamani ya upendo. Hata kama utapata mtu wa kukupenda kwa kiwango gani hutaamini kama kweli anakupenda kwa sababu hujui thamani ya upendo.
Lakini kama ukikutana na mtu ambaye tayari anajua thamani ya upendo kama ujuavyo wewe, mtapendana kupita kiasi . Kila mtu atakuwa anataka kuonyesha upendo kwa mwenzake, na kila mtu atathamini upendo wa mwingine.
Lakini hii kusema bila shaka nakupenda .  hata hivyo tuna watoto pamoja. Huo sio upendo . Hio ni Nira umefungiwa na huna njia ya kutokea , inabidi kusema unampenda sio tu  kwa kuwa upo naye bali unatambua. Kusema kweli upendo unaanzia ndani ya mtu mwenyewe. kama hujipendi wewe. sio rahisi kumpenda mwenzi wako.  Lakini je mnapendana wote wawili?
mxqbsmjedwb1lebyrupc590832b2482bb Utajuaje Kama Mwenza Wako Hakupendi
Utajuaje kama mwenza wako hakupendi kama inavyostahili kupendwa. Mahusiano yenu yatakosa afya. Tabia za hasira , huzuni mara kwa mara japo upo na mwenza wako. utakuwa unaugua mara nyingi kutokana na  stress nyingi .
Njia 6 ambazo zitakuonyesha dalili za kuwepo upendo au kutokuwepo upendo ndani ya mahusiano…
1.Kutokujali
Mwenza anayejihesabia haki, hawezi kumjali mwenza wake, ni mtu ambaye anataka kunyenyekewa kila wakati , kujiona bora kuliko mwenza wake. anapenda kwenda sehemu nzuri peke yake bila mwenza wake. anaweza hata kusafiri peke yake kujifurahisha mwenyewe.
2.Umbali
Wenza wanaopendana mara nyingi watahitaji kuwepo karibu kila mara. Hata kama wanafanya kazi sehemu mbalimbali , wanaweza kutafuta muda wa kuwasiliana au kujitahidi kula chakula cha mchana kwa pamoja. Lakini kama hivi vitu havipo kwako , upendo huo una wasiwasi.
3.Mapenzi Ya Kimwili
Wenza wanaopendana wanafanya sex mara nyingi. kila mmoja anapenda kumfurahisha mwenzake chumbani. Sio hali ya kuatafuta hisia, bali hisia zao ziko sahihi , hamu na thamani .  wanaweka bidii katika kuboresha mapenzi yao.
4. Mtazamo.
Kila mara watu hawa hutafuta mbinu ya kumaintain lengo lao.  kupeana zawadi ndogo ndogo. kila anapoona mwenza wake hana furaha hutafuta mbinu ya kumrudisha katika hali ya kawaida. Lakini kama mwenza wako hayuko kwenye akili yako  inawezekana kabisa hauna mapenzi naye.
5.Thamani.
Wenza wanaopendana  hujiona kama  wana bahati kubwa kukutana na huyo mwenza wake. mara nyingi hufikiri kuwa amekutana na soulmate wake. Lakini kama unafikiri mpenzi wako ni samaki mwingine wa baharini,, huna mapenzi naye.
6.Heshima.
Wenza wanaopendana wanaheshimiana. wanakuwa na hamu kila mmoja kwa mwenzake na hupenda kusaidiana, mbali ya heshima , ni watu wanaosikilizana, wanashauriana na wana maelewano. wanashirikiana kazi zao. Lakini kama unamtreat tofauti na hayo, huenda humpendi.
Kukosekana kati ya hizi sehemu haina maana kuwa kuna uhakika wa lazima kwamba hauko kwenye mapenzi. lakini kama ndio hivyo, lazima uchukulie umakini  ukweli wa mahusiano  yako ili urekebishe mapema  kabla mambo hayajaharibika.

No comments:

Powered by Blogger.