Vitu 8 Vya Kuwa Macho Kabla Ya Ndoa.
Ndoa ni ktu cha muhimu sana kinachobadilisha maisha ya watu wawili wanapoamua kuishi kwa pamoja.
Pale unaposema , Nakubali.
Maisha hubadilika palepale, huwezi tena kuwa yule mtu wa kwanza.
Ndiooo!!.
huwezi kutengana na mwenzio na kwenda kwa mwingine.
Kwa sababu unapoolewa, unapooa huyo mtu anakuwa ni sehemu ya mwili wako na ni sehemu ya maisha yako, kuanzia hapo hadi siku ya kufa, lazima ulielewe hilo mapema. kwa hio nakuletea hapa vitu 8 vya kuwa makini kabla ya ndoa.
1.Lazina kutambua kama wote mko sahihi.
Mara nyingi watu hujikuta wameoana , si kwa ajili ya kupendana kwa dhati , ni vile walikuwa wakikutana kimwili kawaida, kuridhishana kawaida. lakini watu hawa hufika wakati hugundua kuwa hawakutakiwa kuoana. ndoa inakuwa haina amani tena. hata kama walikuwa wanafurahia vipi hilotendo , hawakuwa sahihi kila mmoja.
Kwa maana hii basi , mimi naamini kwamba ni vizuri kufanya tendo hilo ukiwa ndani ya ndoa, kuliko kutengeneza mahusiano kwa ajili ya kufurahishana halafu basi. labda kama ni urafiki tu au ni mazoea ya kawaida.
Jaribu sasa kuangalia hisia za mwenzio, endapo hutafanya nae kitu , atakuaje? mnaweza kuelewana? , je unaweza kucheza nae , kufanya vitu vingi bila ya kufanya tendo la ndoa? bado atakuwa na mapenzi na wewe. maana kuna mwingine nia yake ni moja tu kwako. washa taa yako ya ndani utagundua kama huyo ni wako ama sio.
2.Ni lazima kujua mambo yake ya mwanzo kabla ya kuja kwako.
Kwa swali hili sisemi mapenzi mlionayo, au ni mazoea gani mko nayo, hapana. kuna vitu ambavyo havisemwi kati yenu. hasa mahusiano yaliopita. usidanganye sema ukweli, ulikuwa na mke ukamwacha, uliolewa ukaachika mapema hata kabla ya mwezi , sema mapema . una mtoto ulizaa kabla sema. kuna msichana ulikuwa nae akakuumiza sema, isije baadae ukajulikana hivyo vitu ni bora ukisema inaokoa mambo mengi.
Naesema hivyo kwa sababu , usipokuwa muwazi itakugharimu baadae, hata kama uliwahi kubakwa inabidi kusema, hutapata furaha ukikaa nalo.
3.Chunguza kama mnaheshimiana.
Ndoa haiwezi kuwa nzuri kama hakuna heshima kati yenu,Heshima nin nini basi, ni kuona kuwa mwenzio anastahili, ni muhimu kwako, ni maalumu sana kwako, kitu adimu cha thamani, yupo kwa ajili yako, unatumia muda mwingi kwa ajili yake, kumpa kipaumbele. kama wewe ni mkweli sema ndio. unamheshimu huyo mtu. na kama sio chukua hatua nyingine.
4.Angalia kama anakuona wewe ni peke yako. wa kwake tu.
Tatizo kubwa linalosababisha ndoa nyingi kuvunjika ni usaliti . ni hatari sana , na ni kweli sio sahihi. kwenye kiapo cha ndoa uliahidi kumpenda, kumheshimu na kumfanya awe na furaha kila siku.
Uliahidi kuwa mwaminifu mpaka kufa.
Kama huwezi kutunza hio ahadi , Usioe, usiolewe.
Watu waliooana wanatakiwa kukamilishana wao kila mmoja na hamu zao bila ya msaada wa nje.
Haijalishi utatumia mbinu zipi kutengeneza hilo lakini mtu anaekuoa , unaemuoa lazima akufanyie vitu hivyo, ili usiweze kuhitaji mtu mwingine.
Je huyo ulie nae anakutimizia hayo? ni mume au mke wa kukutosheleza?.
5.Utanipenda nikiwa mgonjwa na nikiwa mzee?
Usiangukie kwa mtu ambae anatafuta kampani, amechoka kuwa peke yake, anayeonekana amechoshwa na muda. ila angalia uzuri uliopo ndani yake. jiweke mwenyewe kwenye viatu vyake.mfano mtu ambae ni mgonjwa wa cancer, utakuwa unampenda wakati wote anaumwa na amepoteza nywele zake zote?
akiwa amezeeka utampenda?
Na kama utampenda mtu kwa sababu yeye ni sex na ana misuli, au ni mzuri na ana umbo zuri, utakuwa umefeli. huo sio upendo. itaisha kwa muda mfupi .
Hakikisha unampenda mtu jinsi alivyo, penda utu wao, penda jinsi ambavyo wanakufanya uwe na furaha wakati unapokuwa na huzuni.
Wapende kwa kila kitu kinachowafanya wao wawe ni wao.
6.Tunayo nafasi?
usipoteze muda kwa watu wengine , huoi au huolewi ili uwe kama wao. unaoa au unaolewa ili kuanzisha timu mpya na tofauti na wengine. wala usifananishe tabia zao na za kwenu, nyie ni tofauti, furahieni vitu kwa pamoja. lakini mwache mwenzako aende kazini kwake na wewe nenda kazini kwako.
hakuna tatizo kufanya kazi sehemu tofauti. jipeni nafasi, kwa kuaminiana kila mmoja.
7.Angalia kama mnasaidiana.
je, unapokuwa na matatizo , unamwona akiwa mstari wa mbele kukusaidia?,, je anapokuhitaji unakuwepo kwa wakati?, maswali haya ni muhimu, jifunze kusaida, ni wamoja inabidi kusaidiana, unatumia nguvu nyingi kumuelimisha na kukuelewa au hapana.
chunguza hivi vitu kujua ugumu uko wapi kabla ya kuingia kwenye agano.
8.Ni mambo yapi huwa hakubaliani.
Kuhusu fedha, watoto na familia inabidi kuongelea mapema,kazi zenu, kupanga watoto wangapi, jinsi ya kutunza rasilimali, matumizi ya fedha yote huongelewa kabla..
Ndoa ni hatua muhimu katika maisha ya kila mwanadamu, kwa hio uwe makini sana na uchague kwa hekima.
Endapo umeoa au umeoolewa unakaribishwa kuongeza maoni yako, na wale ambao bado karibuni kwa maswali.
shirikisha makala hii rafiki na familia yako.
No comments: