Utajuaje Kama Girlfriend Wako Anakupenda ? Dalili Na Ishara Zote Tunazo Hapa

Unaweza kuwa na girlfriend kwa muda mrefu na usiweze kujua kama anakupenda au la. Wanawake wengine wanaweza kujifanya girlfriend wazuri kumbe wanakutumia. Na pia unaweza kuwa na girlfriend halisi ambaye anakupenda kuanzia juu mpaka chini.

Kama mwanaume, unapaswa kujua ishara zote ambazo zinaonyesha iwapo mwanamke anakupenda ama anakutenda. Hii ni muhimu kwa kuwa utakuwa unasoma vigezo vyake ili uweke uamuzi wa mwisho kama iwapo utakubali kuishi na yeye milele ama utaamua kumuacha katikati.

Hapa Nesi Mapenzi leo tumekuletea ishara zote ambazo zitakuonyesha iwapo mwanamke/girlfriend wako anakupenda au la. Zama nasi.

Ishara kuonyesha kama mwanamke/girlfriend wako anakupenda.


#1 Anakufanyia yale mambo madogo madogo kuyafanya maisha yako kuwa rahisi. Kama mwanamke anakupenda basi jambo la kwanza la kufanya ni kuonyesha upendo kwa anayempenda. Kama unamwona anakukunjia nguo zako, anakutembelea kuhakikisha nyumba yako iko safi ama kuhakikisha hausahau kununua kitu muhimu kwa nyumba yako basi ujue anakupenda.

#2 Anakuoshea nguo. Kama anakufanyia kitu nyumbani kwako ambacho yeye mwenyewe huwa hapendi kufanya kwake basi ni ishara nzuri. Anajaribu kuonyesha uanawake wake kinyumba. Katika DNA ya mwanamke ni kuwa ameumbwa kuwajali wale ambao anawapenda ili kuwarahisia maisha. Kama girlfriend wako anaonyesha hizi tabia basi ujue anakupenda.

#3 Kando na kuwa anajua chakula unachokipenda, anajaribu kukitengeneza. Anajua chakula nachokipenda? Ashawahi kukutengezea mara kwa mara? Huyo anakuonyesha kuwa anakupenda.

#4 Anaelewana na familia na marafiki zako hata kama hawamthamini. Kama girlfriend wako anatabasamu hata kama familia yako inachukiza, basi huo ni upendo. Kwa kawaida wanawake hawaelewani na familia ya mwanaume. Lakini ukiona anajaribu bila kulalamika, hio ni ishara ya upendo kwako.

#5 Anakatiza shughli zake kuja kukuona. Kama yuko tayari kuuza tiketi yake ya kwenda kwa concert ya Diamond ili aspend usiku na wewe, hio ni ishara ya kukuambia, "nakupenda."

#6 Anayaweka matakwa yako mbele. Ukiona yuko tayari kufunja sherehe na marafiki zake ili asherehekee na familia yako ama kwenda kula dinner na marafiki zako ni ishara ya mapenzi.

#7 Anakusifia pale ambapo inahitajika. Mwanamke ambaye anakupenda hataona tatizo kukusifia pale ambapo kunahitajika. Kuambia mtu kuwa unampenda kunaonyesha kuwa unamthamini.

#8 Ni mtu wa kwanza kukupigia iwapo ana furaha, huzuni ama hasira. Kitu chochote ambacho kitamtokea yeye atakuwa wa kwanza kukuambia. Hii inamaanisha anakupenda na anakuamini. Uwepo wako kwake anaudhamini na kuuzingatia.

#9 Atakwambia mambo ambayo hayapenda. Ashawahi kukuambia mambo yaliyomuaibisha, huzunisha ama kumfelisha? Ukiona anakwambia kila kitu hata siri zake za kuzimu basi fahamu kuwa anakupenda.

#10 Anaonyesha ukichaa wake. Hakuna mtu anaweza kufunguka asilimia 100 tabia zake kwa yeyote. Ukiona amekuwa huru na wewe kiasi cha kuwa anaweza kuachilia hewa, kukuonyesha sura za kiajabu, ama kufanya mambo ambayo hukutarajia, basi ni ishara ya kuwa penzi lake kwako ni la dhati.

#11 Anashikwa na wivu ukiongea kuhusu wanawake wengine, lakini si sana. Mwanamke anayekupenda huwa hapendi kuskia ukiwasifu wanawake wengine. Hio ni kawaida.

Hizi ni baadhi ya dalili kuonyesha kuwa mwanamke anakupenda. Je girlfriend wako anaonyesha hizi tabia ama ni mtofauti na tabia hizi tulizozitaja? Uamuzi ni wako sasa.



No comments:

Powered by Blogger.