Dalili Saba kwamba Mke/Mpenzi wako Hujamfikisha kileleni

Related image

Katika mahusiano ya kimapenzi tendo la ndoa ndiyo kitu kikubwa kabisa ambacho kinamuunganisha mwanaume na mwanamke, nilazima kila mmoja kufurahia tendo la ndoa la sivyo hakutakua na furaha ndani ya hayo mahusiano. Ni jukumu la mwanaume kuhakikisha hili linafanyika, lakini ni kwa bahati mbaya sana kuwa katika kufanya mapenzi wanaume wengi huwa wabinafsi na kujiridhisha wao tu, baadhi hufanya kwa kujua huku wengi wakiwa hawajui kua pamoja na juhudi zao zote hawawaridhishi wapenzi wao.
Kwa mwanaume akiwa na nguvu za kiume na akiweza kufunga magoli kadhaaa hujiona kidume na naaporidhika basi kwake kila kitu hukiona sawa akidhani kua na mwenza wake karidhika. Takwimu zinaonyesha kuwa takribani aislimia 70 ya wanawake hawafiki kileleni na wengine hawajui hata maana ya kufika kileleni. Kuna mambo mengi ambayo husababisha lakini kubwa ni ubinafsi wa wanaume, wanaume kutokujua na mambo mengine kama hayo.
Kwa mwanamke ambaye hajawahi kufika kileleni katika maisha yake inaweza kuwa sawa, asione kama kuna tatizo akijua anachofanyiwa na mwenza wake ndiyo kinachopaswa kufanywa lakini kama alishawahi kufika na akakutana na mwanaume ambaye hamfikishi kileleni basi hilo ni tatizo. Lakini hata kama hakuwahi kufika siku akichepuka kidogo akapata mtu wa kumfikisha huko basi ni rahisi kumganda hivyo mwanaume unatakiwa ujue kua unamfikisha mwenza wako au la, zifuatazo ni dalili kua mwanaume humfikishi mwenza wako kileleni;
(1) Unaaza Kukoroma Kabla Yake/Mkimaliza Mchezo Anataka Kulala; Hii inaweza kuwa dalili ya kwanza kabisa kua kazi unayofanya siyo, inaweza kuwa hivi kila mnapomaliza kufanya mapenzi dakika mbili umechoka umelala unamuacha macho anashangaa, hakuna hata ile after sex, hakuna hata romance baada ya sex, umechoka na unamuacha macho, kama inatokea hivi mara kwa mara, dakika kadhaa unakoroma basi jua mwenzako alikua hajafika na umemuacha na maumivu.
Lakini kuna wengine ambao, unamaliza mambo yako, unajiona umefanya kazi ngumu lakini hulali lakini unapomalizi tu hataki hata umguse, anakua kama ana hasira flani hivi, huwezi kumkumbatia na romance kidogo. Hajachoka lakini anageukia upande mwingine anajifanya kulala. Hapa jua ana hasira kwakua ni kama umemshikashika na kumpandishia mizuka yake halafu hujamridhisha, yuko katika maumivu na anakua hataki kuongea na wewe kwani unamboa.
(2) Hataki Kufanya Mapenzi Na Wewe; Kila siku anakua kama vile ana hasira, unamtaka lakini hakutaki, achana na kile kitu cha mara moja kwamba hayuko kwenye mood, hapana yeye ni kila siku hayuko kwenye mood. Ukigusia suala la kufanya mapenzi atatafuta sababu yoyote ile ili asifanye na wewe. Hii ni dalili kuwa haridhiki, kitendo cha wewe kila siku kumchezea na humfurahishi kinamfanya kuhisi kama kila sikua anabakwa hivyo kukosa hamu ya kufanya mapenzi.
Mwanamke ni kama mwanaume tu nao wanahamu, kama unampa shughuli nzito basi akikuona anasisimkwa tu akiwaza hata bila kumgusa. Lakini kama hamna kitu nilazima atakua na hasira na atatafuta visingizio msifanye mapenzi kwakua tu hataki kushikwashikwa na kuachwa. Kama kila siku mwenza wako hana hamu na usipomuambia wewe anaweza kukaa hata mwezi bila kuhitaji, usikimbilie kuwaza kuwa anachepuka hapana wakati mwingine ni kama kachoka, hisia hana tena anaona ni kujitesa tu kufanya mapenzi na wewe.
(3) Analalamika Maumivu Mara Kwa Mara; Kila wakati mkifanya mapenzi analalamika maumivu, hii ni dalili kuwa humuandai vizuri, unamuacha mkavu hivyo unapokua unatimiza majukumu yako basi unamuumiza. Mwanamke kama huyu hawezi kufurahia tendo la ndoa kwani, mbali na yale maumivu ambayo hayapata wakati wa tendo lenyewe lakini ile hali huathiri akili yake pia kule kuwaza kuwa usiku nitakua na mtu flani na sitafurahia inamuondolea mood na kumuondolea uwezekano wa kufika kileleni.
(4) Analalamika Anakupa Maelekezo Wakati Wa Tendo La Ndoa Au Baada; Hiki ni kitu kizuri na kama mwanaume utaacha mihasira yako na kutokujiamini basi unaweza kuibadilisha hali. Unafanya naye mapenzi kila wakati anakuambia fanya hiki, nishike hapo, rudi huku, tubadilishe staili hii. Lakini baada ya tendo lenyewe anakuambia nilifurahi ulipofanya hiki, napenda mikono yako ikitembea hivi na mambo kama hayo. Hii ni dalili kuwa inawezekana humfikishi au humkuni vizuri na ni kwakua hujui hisia zake ziko wapi.
Anachofanya ni kama kukuelekeza kuwa usitafute rimoti juu ya bati wakati iko juu ya kochi. Sijui mmenipata, anaona unajitahidi kishika sehemu moja na yeye anajua hisia zake ziko sehemu nyingine hivyo anajua hutamfikisha na anakuelekeza. Kama ukifuatilia maelekezo yake vizuri basi itakua rahisi kumfikisha kuliko kukasirika. Lakini jua tu kama kila siku anakupa maelekezo jua kuna kitu unakosea hivyo jaribu kukifanyia kazi ili umridhishe.
(5) Haonyeshi Ushirikiano Wakati Wa Tendo La Ndoa/Anakua Na Hasira;Wakati mwingine unaweza kudhani kua unafanya mapenzi na Gogo, hajitingishi, anakua kama anafuata malekezo yako tu, hufanya pale ambapo wewe unataka na hata mkimaliza hajali kilichotokea. Katika kubadilisha staili ni hajali, amelala tu hashughuliki, kila kitu unajikuta unafanya wewe mwenye. Mwanzo alikua anajitahidi hata alikua anatoa maelekezo alikua analazimishia romance lakini sasa kabadilika.
Iko hivi mwanzoni labda ulikua unamfikisha ndiyo maana alikua anaonyesha ushirikiano na sasa hujali, au mwanzoni hukua unamfikisha lakini ilikua mwanzo hivyo alikua anajipa moyo kuwa mambo yatabadilika, labda mkizoea na atakupenda na atafika. Lakini hakuna kilichobadilika, mambo ndiyo yanazidi kuwa mabaya zaidi hivyo anakata tamaa. Anaanza kuwa na hasira hata katika maisha tu ya kawaida, hasira kwako, watoto na wageni, ni kama anona kila mtu anamsaliti, ana mawazo sana.
(6) Anajishika zaidi kuliko wewe unavyomshiika; Wakati wa tendo la ndoa unakuta mikono yake iko bize sana, anajishika sehemu ambazo wewe mwanaume ndiyo ulitakiwa kuzishika, anauchezea mwili wake sehemu ambazo ulitakiwa kuchezea wakati wa mechi, kifuani kiunoni na kule chini. Lakini hata baada ya kumaliza unakuta haachi anaendelea kujichezea, hii ni dalili kuwa humkuni vizuri, hajafika lakini kwakua wewe umemaliza hana namna ni bora ajimalizie mwenyewe ni kama vile anafanya musterbation wakati mkifanya mapenzi!
(7) Hajali Tena Yeye Kuridhika; Kila wakati anataka kukufanyia mambo wewe uridhike, yuko tayari akufanyie kila kitu lakini hajali kama na wewe unamfanyia chochote, anataka kufanya staili ambazo unazipenda wewe, anataka kufanya mambo ambayo unayapenda wewe na namna ambavyo unapenda. Wakati mwingine anakuuliza kama umeridhika, huku yeye ukiona kabisa hajaridhika au hajijali. Unaweza kuona labda ni upendo lakini wakati mwingine nikua yeye kashakata tamaa kufika kileleni na anaona ni bora kukuridhisha wewe tu!
Mwisho nimalizie kwa kusema kua, wanawake wanajua kua kama ukimuambia mwanaume hakufikishi basi atajisikia vibaya, kuwa na hasira na hata kumuona mwanamke Malaya. Hivyo ni ngumu sana kwa mpenzi wako kukuambia kuwa hujamfikisha kileleni hivyo ni kazi yako mwanaume kujua. Hata kama una matatizo flani, kukasirika kasirika na kuacha kumsikiliza hakusidii, jitume na fanya mambo mengine ya ziada, romance ni ya muhimu kwani humuandaa mwanamke kwaajili ya kukupokea na kumsaidia kufika kileleni mapema.



No comments:

Powered by Blogger.