NJIA MAHSUSI ZA KUMFANYA MWANAUME AWE NA MVUTO WA PEKEE KWA MWANAMKE.
Kuna msemo wa kiingereza usemao “Nothing comes from vacuum” wakimaanisha kwamba hakuna kitu kichokuwa na chanzo chake au hakuna jambo linalotokea tu pasipo kuwa na chimbuko lake.
Msemo huu tunaweza kuuleta hata katika mapenzi pale tunapomwona mwanaume fulani anapendwa sanaa na wanawake hapa nazungumzia kupenda sio kule kutamani eti labda sababu ya pesa au mali alizonazo.
Mwanaume mwenye uwezekano mkubwa sana wa kupendwa kwa dhati ni Yule mwenye mambo yafuatayo:-
*Mwanaume mwenye tabia nzuri inayokubalika katika jamii kama vile upendo,ukarimu,ustaarabu na mambo mengine mengi ambayo binadamu wa kawaida hujisikia faraja au furaha sana akifanyiwa,hivyo mwanamke hujisikia amani sana kuwa na mtu wa namna hii sio Yule mwanaume mwenye roho ngumu,hana huruma,upendo nk.
*Mwanaume mwenye kauli nzuri,hii ni sifa nyingine ambayo kwa kiasi kikubwa hupendwa sana na watu wote,hata kwa upande wa wanawake hupata amani sana kukutana na watu wa aina hii kuliko watu wenye kauli chafu,matusi,kashfa nk. Hivyo ukiwa na kauli nzuri ujue una asilimia kubwa ya kupendwa sana na wanawake wa kila aina.
*Mwanaume mwenye muonekano mzuri ki mavazi,hii ni sifa nyingine matata ambayo wanawake wengi sana hupenda wanaume wao wawenayo. Mwanamke mara zote hupendelea zaidi mtu smart ambaye anajitunza.
*Awe mwenye tabasam lenye kuvutia,asiye na dharau na mcheshi kiasi.UWE MWANGALIFU USIJEUKAPITA KIASI!
*Zungumza LAKINI usitawale mazungumzo
*Uliza maswali LAKINI usimchimbe mtu
*Onyesha urafiki LAKINI usicheze-cheze kimapenzi
*Jiamini LAKINI usijigambe
No comments: