MZUNGUKO WA HEDHI NA MATATIZO YAKE

Image result for siku za hatari kushika mimba

 
FAHAMU KUHUSU MZUNGUKO WA HEDHI NA MATATIZO YAKE (MENSTRUATION)
Habari za leo ndugu Rafiki uliyeamua kuungana Nami kufanikisha zoezi hili la kuwasaidia wakina mama na wasichana wengi kupata elimu ili waweze kudumisha afya yao na kupata mzunguko wa hedhi ulio salama, napenda kukushukuru na kukuomba uendelee kuwa Nami kuweza kuwasaidia wakina mama na mungu atatulipa kutokana na juhudi zetu kuwasaidia wenye uhitaji
NINI MAANA YA MZUNGUKO WA HEDHI??

Ni mzunguko wa kila mwezi ambao husababisha kutokwa kwa damu kila mwezi ukeni kutokana na mimba kutotungwa,
~mzunguko wa damu umegawanyika katika maeneo makuu mawili( 1)MZUNGUKO WA DAMU UNAOPEVUSHA MAYAI (OVULATORY CYCLE)
(2)MZUNGUKO WA DAMU USIOPEVUSHA MAYAI (ANOVULATORY CYCLE)
Napenda tufahamu kwa kina mizunguko hii
MZUNGUKO WA HEDHI UNAOPEVUSHA MAYAI (OVULATORY CYCLE) ~katika mzunguko huu mwanamke hutokwa na ute ute wa Uzazi ambao unavutika na katika mzunguko huu mtu anaweza kupata ujauzito
MZUNGUKO WA HEDHI USIOPEVUSHA MAYAI (ANOVULATORY CYCLE) ~katika mzunguko huu mwanamke hatoki ute ute wa Uzazi hivyo hawezi kupata ujauzito

~ pamoja na mizunguko hii miwili kutofautiana mwanamke hupata hedhi kama kawaida hata hivyo mwanamke ambaye mzunguko wake wa Hedhi hapati ute ute wa Uzazi hawezi kupata ujauzito kutokana na mabadiliko ya mfumo wa homoni
pia napenda mfaham kuwa ute ute wa Uzazi umegawanyika katika Makundi makuu matatu ambayo ni (1)UTE MWEPESI
(2)UTE UNAOVUTIKA
(3)UTE MZITO
Mara nyingi wanawake wasiopevusha mayai hawawezi kupata ujauzito hivyo huwa hawapati ute wa Uzazi na pia wengine hupata ute mzito daima kama uchafu unaotoka ukeni Lakini wenyewe hauna harufu wala muwasho
JINSI YA KUTAMBUA MZUNGUKO WAKO WA HEDHI
~Kila mwezi ovari za mwanamke huzalisha yai moja ambalo Lina uwezo wa kukaa kwa muda wa masaa 36 ndani ya mirija ya Uzazi hivyo inapotokea yai hili halijarutubishwa ukuta wa mji wa Uzazi hubomoka na kutoka nje ya uke pamoja na damu kwa neno Moja tunasema siku za hedhi,
mzunguko wa hedhi huanza kuhesabiwa siku ya kwanza mwanamke anapoanza kupata siku zake,
Pia mzunguko wa hedhi uwe unaopevusha mayai au usiopevusha umegawanyika katika Makundi ya mizunguko mitatu yani MZUNGUKO MFUPI, MREFU NA WA KAWAIDA
~(1)MZUNGUKO MFUPI ~huu ni mzunguko wa siku 22_27
~(2)MZUNGUKO MREFU ~huu ni mzunguko wa siku 31_35
~(3)MZUNGUKO WA KAWAIDA ~huu ni mzunguko wa siku 28_30

JINSI YA KUSOMA MZUNGUKO WAKO
Tuchukulie mzunguko mfupi ambao ni siku 28
~siku ya kwanza mpaka ya tano huwa ni kipindi cha mwanamke kuingia katika mzunguko hivyo ni mwanzo wa mzunguko katika kipindi hiki ukuta wa mji wa mimba hubomoka na kutoka nnje pamoja na damu ukeni (siku ya hedhi) Katika kipindi hiki homoni za estrogen na progesterone huwa ndogo pia katika kipindi cha siku ya 6_10 ni kipindi ambacho ukuta wa Uzazi huanza kujengwa Tena kwa ajil ya kupokea kiini tete kipindi hiki mwanamke hawezi kupata mimba ila ni kipindi ambacho kinaelekea katika hatari hivyo katika kipindi hiki homoni za oestrogen huwa nyingi hivyo katika kipindi hiki yai huzalishwa (ovulation) siku ya kumi na moja ya mzunguko pia huweza kukaa kwa muda wa masaa 36 yani hutoka katika ovari na kusafiri katika mirija ya falopia mpaka siku ya kumi na nane na katika kipindi hiki homoni ya progesterone huzalishwa kwa wingi kwa ajili ya kutunza mji wa mimba pia homoni ya progesterone hupungua mwishoni mwa mzunguko yani kupungua huku husababisha mwanamke kuingia Tena katika mzunguko wa hedhi
~kipindi ambacho mwanamke ana breed hupata damu ya rangi nyekundu na huwa Ina mabonge kias kidogo na hutoka kiasi cha ML 35_50 kwa saa.
~kwa Kawaida ni kitu kizuri na cha kufurahia mwanamke kuona breed ila kutokana na matatizo wanayokutana nayo wanawake hujikuta wakichukia kuona siku zao kutokana na maumivu au adha mbalimbali wazipatazo. Ambazo ni
(1)MAUMIVU MAKALI WAKATI WA HEDHI
(2)KUKOSA HEDHI AU KUPATA KATIKA MPANGILIO USIO SAHIHI
(3)KUTOKWA NA DAMU NYINGI
Leo tuanzie hili suala la maumivu makali wakati wa hedhi na namna ya kutatua
MAUMIVU MAKALI WAKATI WA HEDHI (DYSMENORHOEA)
Kwa ushauri zaidi wasiliana kwa kutuma message namba hizi:
0765203999 BASSA MUSSA

No comments:

Powered by Blogger.