Urembo wa vikuku, vishaufu na cheni (shanga) kiunoni kwa wadada
urembo huu ulionekana zaidi katika baadhi ya makabila ya kiafrika ukivaliwa na watu wa rika zote; kuanzia watoto wachanga, wasichana, wanawake wa makamo, hata wazee.
Kwa baadhi ya makabila hayo, vikuku vimekuwa vikivaliwa kama mila kwamba kila mwanamke anapozaliwa lazima avae urembo huo kwa kufuata desturi na tamaduni zao, tofauti na ilivyo sasa ambapo wengi huvaa kama urembo wa kawaida.
Vikuku hivyo vyaweza kuwa vya shanga, ngozi au hata madini kama dhahabu, fedha na shaba. Kikuu kinaweza kuvaliwa mguu mmoja au miguu yote.
Wanajaamii wengi wamekuwa na mtazamo tofauti kuhusu uvaaji wa vikuku wakihusisha na mambo yasiyofaa na kuonyesha kuwa wengi wanaovaa urembo huo wamepotoka, au kwenda kinyume na maadili ya kitanzania.
Hata hivyo, wapo baadhi ya watu ambao ni wadau wa urembo wanafafanua kuwa pambo hilo halina maana yoyote livaliwapo kwenye miguu ya mwanamke zaidi ya urembo kama ilivyo kwa hereni na mikufu.
"Watu wanashindwa kuelewa kuwa kikuku ni urembo wa mwanamke kama ulivyo urembo mwingine, mfano bangili, hereni, cheni ya shingoni, pete ,vidani na mapambo mengine ambayo hupenda kujiweka mwilini, unajua mwanamke kujipamba,"anasema Nice Siema
Anafafanua kuwa uvaaji wa urembo huo hauwezi kutafsiri tabia ya mtu kwa kuwa ni pambo kama yalivyo mapambo mengine yanayotumiwa na wanawake.
"Unajua siku zote wanawake wanapenda kupendeza ndiyo maana huwa na furaha kama sehemu kubwa ya miili yao wataiweka urembo tunaona hata vidole vya miguu vinavalishwa pete hiyo yote ni urembo tu hakuna maana yoyote mbaya,"anasema Siema
Kwa mujibu wa wadau wa urembo kikuku kinapaswa kilegee kidogo katika mguu na kwamba hakipendezi kikiwa kimebana, kwani licha ya kusababisha matatizo katika kuruhusu damu kutembea, hakiwezi kuwa na mwonekano mzuri kikiwa katika hali hiyo.
Bila shaka katika mitindo inayoonekana kupokelewa vizuri na wanawake hasa wasichana ni pamoja na uvaaji wa vikuku ambao sasa umetikisa katika kila nyanja.Suala la urembo kwa sisi wanawake linjumuisha mambo mengi sana kuanzia mavazi na hereni, vishaufu bangili vidani na makochokocho mengine.
Siku za karibuni kumeibuka mtindo wa wanawake kuvaa vikuku yaani cheni za miguuni. jambo hilo limekuwa likipigiwa kelele na baadhi ya watu wenye mrengo tofauti wakihusisha jambo hilo na tabia zisizofaa.
Lakini cha kushangaza nimewahi kuona baadhi ya wabunge wanawake na viongozi wa kike serikalini tena wenye mamlaka makubwa wakiwa wamevaa vikuku tena wengine walipata hata fursa ya kupiga picha na mkuu wetu na vikuku vyao.
Ninachofahamu mimi, bungeni ni mahali ambapo mavazi yanazingatiwa sana, na ninaamini wengi wetu tumewahi kushuhudia baadhi wabunge wakitolewa nje kwa sababu ya mavazi yao kuonekana kwenda kinyume na matakwa ya bunge, lakini pamoja na jamii huku nje kuwahukumu wanawake wanaovaa vikuku kama watu waliopotoka kimaadili, lakini kwenye eneo hilo la bunge inaonekana jambo hilo limepewa Baraka.
Sasa kwa kuwa suala la urembo kwa wanawake linaenda na wakati, hivi sasa tumerudi Kiafrika Zaidi, na sasa urembo wa shanga umechukua nafasi. licha ya shanga kutumika kama chachandu ya kunogesha mapenzi kwa kuvaliwa kiunoni na wanawake, lakini kwa miaka mingi urembo wa shanga umekuwa ukitumiwa na waafrika wake kwa waume katika kujipamba.
Mfano mzuri ni kwa Wamasai ambao kwa miaka mingi wamekuwa wakijipamba kwa shanga wake kwa waume na wamekuwa wakipendeza haswa
Urembo wa vikuku, vishaufu na cheni (shanga) kiunoni kwa wadada
Reviewed by Bassa
on
8:01 AM
Rating: 5
No comments: